Saturday, 22 July 2017

Magoli ya Mbwana Samatta na Wayne Rooney timu zao zilipokutana leo


Jumamosi ya July 22 2017 mtanzania Mbwana Samatta alipata nafasi ya kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton FC inayodhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.
Mchezo wa Everton dhidi ya KRC Genk uliyochezwa nchini Ubelgiji katika uwanja wa Luminus Arena, umempa nafasi nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta kuonesha uwezo wake dhidi ya Everton ambayo ni miongoni mwa vilabu saba England ambavyo havijawahi kushuka daraja toka kuanzishwa kwa mfumo wa Ligi Kuu England 1992.
Mbwana Samatta ambaye ndio mshambuliaji tegemeo wa KRC Genk baada ya kuumia kwa mgiriki Nikolaos Karelis aliifungia KRC Genk goli la kusawazisha dakika ya 55, hiyo ni baada ya Wayne Rooney kuifungia Everton goli la kwanza dakika ya 45 kwa kutumia vyema assist ya Sandro Ramirez.




Genk vs Everton All Goals & Highlights HD 22.07.2017 Friendly

Related Posts:

  • Wachezaji bongo tusiogope kwenda nje - MaguliMshambuliaji wa kimataifa anayeitumikia klabu ya Dhofar SC ya nchini Oman, Elias Maguli amewataka vijana wa Kitanzania wanaotaka kuendeleza vipaji vyao, nje ya nchi kujaribu pale wanapopata nafasi na sio kukata tamaa.Maguli a… Read More
  • Manny Pacquiao kuzipiga jumapiliManny Pacquiao (kushoto) akinyoosha mkono wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea pambano lake kutetea mkanda wake wa WBO uzito wa Welter dhidi ya Jeff Horn (kulia) mjini Brisbane, Jumapili… Read More
  • Sijasaini mkataba Simba - AishiMlinda mlango wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Aishi Salum Manula, amekanusha kusaini na Klabu ya Simba huku akiongeza kuwa vipo vilabu vingi vya hapa nchini alivyofanya navyo mazungumzo na muda ukifika itajulikana na … Read More
  • Breaking News: Jamali Malinzi hatoweza kushiriki uchaguzi TFFRais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais.Malinzi hataweza kwa kuwa kesi iliyomfikisha mahakamani leo itasikilizwa tena Jumatatu Julai 3 na Malinzi atakaa rumande hadi siku hiyo.Usaili wa viongozi wanao… Read More
  • Okwi Atema ChecheMshambuliaji wa zamani wa kikosi cha Simba Emmanuel Okwi ambaye jana amerejea rasmi katika kikosi hicho baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Simba amefunguka na kusema amekuja kupambana kuhakikisha kuwa Simba inapata ubingw… Read More

0 comments:

Post a Comment