Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limeendelea na msako maalum ya tokomoza uhalifu na kufanikiwa kukamata Bunduki tatu aina ya Gobore na risasi 54 misokoto 2601 ya Bangi, pikipiki tatu na samani za maofisini na majumbani zilizoibiwa huku watuhumiwa 45 wakishikiliwa kuhusika na uhalifu huo.
Akizungumzia msako huo ambao hauna ukomo kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma SACP Lazaro Mambosasa anasema katika matukio ya wahalifu wa silaha jeshi hilo kwa kushirikiana na idara wanyamapori wamekamata magobore matatu yaliyotengenezwa kienyeji na risasi zake 54.
Kupitia msako huo pia polisi wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 14 na misokoto 2601 ya bangi huku mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Herison Kimbanga mkazi wa kihonda morogoro akikamatwa kwa kuhusika na uhalifu wa kuwawekea wanawake dawa za kulevya kwenye vinywaji na kisha kuwabaka na kuiba vitu mbalimbali.
Aidha kamanda mambosasa amewataka wakazi wa mkoa wa dodoma ambao wameibiwa vitu mbalimbali kujitokeza kwenye ofisi yake wakiwa na nyaraka muhimu ili kutambua endapo bidhaa zao ni miongoni mwa zilizokamatwa
0 comments:
Post a Comment