Saturday, 22 July 2017

Mkuu wa Mkoa atoa agizo katika maandalizi ya kuanzisha viwanda Manyara



Mkuu wa mkoa wa manyara dkt joel bendera ameagiza wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi katika halmashauri zote za mkoa huo kuchagua zao la aina moja kulingana na hali ya hewa katika wilaya zao pamoja na kufanya uhamasishaji kwa wananchi kuanza kulima zao hilo ikiwa ni maandalizi ya jumla ya viwanda vinne viunavyotarajiwa kuanzishwa katika maeneo wilaya nne za mkoa huo.

Ni agizo ambalo Mkuu wa mkoa wa manyara dkt joel Bendera analitoa akiwa katika wilaya ya simanjiro kwa uongozi wa halmashauri hiio huku kiwanda cha kusindika nyama pamoja na ngozi zikitajwa kuwa mbioni kuanzishwa wilayani hapa.

Hata hivyo katika kikao hiki cha madiwani likajitokeza suala la ukwepaji kodi unaofanywa na wafanyabiashara ya madini ya tanzanite hivyo kuikosesha halmashauri hii mapato yake pamoja na serikali huku biashara ya madini hayo ikiendelea kufanyika arusha na Mkoa wa Kilimanjaro badala ya wilaya ya simanjiro mkoa wa Manyara.

0 comments:

Post a Comment