Sababu ya Moyo Kupanuka

Moyo kupanuka au kuwa mkubwa ni tatizo ambalo huathiri utendaji wa mfumo wa usambazaji damu mwilini..

Jinsi ya kukabiliana na vidonda vya tumbo

Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika mwili unaohusika na umeng’enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili ili kuuwezesha kufanya kazi mbalimbali.

Jinsi ya kujiukinga na ugonjwa wa kaswende

Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Ugonjwa wa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Friday 8 June 2018

Waraka wa KKKT....Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini Asimamishwa Kazi.



DAR: Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba

Bi. Merlin amesimamishwa leo Juni 08 ili kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) liliandikiwa barua kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia kwa Msajili wa Vyama na kupewa siku 10 kufuta Waraka wake

Wednesday 6 June 2018

Athari Za Kuwa Na Mipango Mingi Kwa Wakati Mmoja


Moja ya changamoto kubwa ya kushindwa kufanikiwa ni kutokujua unataka nini katika Maisha yako. Huenda ukawa haujanielewa ngoja nikueleweshe, ni hivi unakuta mtu anaona maisha hayaendi vizuri mwisho wa siku ukimuuliza mtu huyo anataka kufanya nini, bila shaka kwa kuwa mtu huyo hajui kile anachokitaka atakwambia kazi yeyote ile mimi nafanya.

Ukiangalia juu ya kauli hiyo ni sawa, mtu huyo huenda akawa sawa hii ni kutokana na hali yake aliyonayo. Lakini katika kununi ya kimafanikio hakuna majibu ya kusema unataka kufanya chochote kile. Ila ni lazima ujue unataka kufanya nini. Moja ya majonzi ya watu waliofeli kimaisha ni kwamba walichanganya vitu vingi kwa wakati mmoja.

Tujifunze kitu kupitia hadithi ifuatavyo.
Hapo zamani za kale kulikuwepo na mfugaji fulani katika kijiji fulani. Na mfugaji huyo alijipatia umaarufu mkubwa sana kijinini hapo hii ni kutokana alivyobobea katika shughuli hiyo, na kutokana na umaarufu huo aliweza kulinda heshima ya jina lake na kuongeza idadi kubwa ya mifugo.

Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo na mifugo ilivyozidi kuongezeka miaka na miaka, hata hivyo kama ilivyo kwa jongoo kuwa na miguu mingi bila macho ni sawa na bure hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mfugaji huyo kutokana na ufugaji hakutaka hata siku moja kumuuza hata mnyama mmoja kwa sababu aliweka malengo yake ya muda mrefu na kuamini ipo siku atakuja kuwa na pesa nyingi na kuwa tajiri mkubwa zaidi kijijini hapo.

Hata hivyo kutokana imani hiyo aliyokuwa nayo furaha na umarufu uligeuka kilio na majonzi hasa pale ulipo ingia ugonjwa wa bonde la ufa (Rift valley) kijijini hapo. Ugonjwa huo uliweza kuangamiza idadi kubwa ya wanyama aliowamiliki mpaka akabakiwa na ng'ombe mmoja.

Mfugaji alinung'unika sana lakini alimbidi akubaline na hali hiyo ambayo imetokea. Hivyo akaamua kumuhudumia yule ng'ombe kama mtoto wake kwani kila alichokihitaji ng'ombe yule alikipata kutoka kwa mfugaji huyo. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya mfugaji na ng'ombe yalivyokuwa.

Siku moja alfajiri mfugaji aliamua kwenda na ng'ombe wake sehemu ambayo ng'ombe yule alikunywa maji kama ilivyokuwa ratiba ya mfugaji yule kila siku. Wakati wanaelekea katika eneo hilo ghafla mbele aliona kiatu, kiatu ambacho kilikuwa ni kizuri sana, aliamua kukichukua kiatu kile na kukiangalia na kuona kinamtosha vizuri baadae ilishangaa mbona kiatu kizuri kiasi kilikuwepo pale barabarani wakati anajiuliza hayo aling'aza macho yake huku na huko lakini hakuona kiatu kingine cha mguu mwingine.

Kwa kuwa hakuona kiatu kingine aliamua kuachana na kiatu kile na kuondoka na ng'ombe wake. Mfugaji aliendelea na safari yake kwa mwendo mrefu sana lakini kadri alivyozidi kwenda ghafla alikutana na kiatu kingine cha mguu mwingine ambacho kinafanana na kile alichokiacha awali. Mfugaji alifurahi sana hivyo alimua akiache kiatu kile cha pili pamoja na ng'ombe mahali pale na kurudi kwa kasi sana kwenda kuchukua kiatu kingine.

Lakini cha ajabu kilichomkuta ni kwamba baada ya kwenda mahali pale kilipokuwepo kiatu cha mwanzo hakukiona kiatu kile, alijaribu kukitafuta sana kiatu kile lakini hakukipata hivyo aliamua kurudi mwanzo ambako aliamuacha ng'ombe na kiatu cha pili lakini cha kushanganza ni kwamba hata huko hakumkuta ng'ombe wala kiatu kile. Mfugaji alilia sana kwa sababu alimpoteza ng'ombe wake ambaye alibaki mmoja na aliyempenda sana. Mwisho wa siku alikosa vyote.

TAFSIRI YA HADITHI HII NI NINI?
Tafsiri ya hadithi hii ni kwamba watu wengi ni wazuri wa kimawazo na kuchangamkia fursa mbalimbali ila changamoto kubwa inakuja hasa pale ambapo unataka mafanikio ya haraka hivyo unajikuta unaingia katika sakata la kuchanganya mambo mengi kwa wakati mmoja.

Mwisho wa siku unajikuta unafanya kitu hiki unaacha mara unafanya kitu kingene kama alivyofanya mfugaji na mwisho wa siku akajikuta anakosa yote. Hivyo ni wakati muafaka leo wa kujua unataka kufanya nini na kukimalisha na sio kuwa na maisha yakutaka mambo mengi kwa pupa pupa na mwisho kukosa vyote. Kuwa mtu chanya ili kupata mafanikio ya kweli.

Monday 2 April 2018

Isome HAPA Barua ya Profesa Kitila Mkumbo Kwenda kwa Mkuu wa Kanisa la KKKT Ikipinga Waraka Wao


Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo,
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
S. L. P. 3033
ARUSHA.

Mheshimiwa Baba Askofu, Shalom!

YAH: MAMBO MATANO AMBAYO HAYAPONYI KATIKA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT

Jina langu ni Kitila Mkumbo, muumini katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambalo wewe ndiye mkuu wake. Kikazi, mimi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Dodoma. Kitaaluma, mimi ni mhadhiri mwandamizi katika Saikolojia na Elimu nikiwa na cheo cha Profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mheshimiwa Baba Askofu, kwa unyenyekevu mkubwa nimeamua kukuandika barua hii ili kutoa maoni yangu binafsi kwa kanisa unaloliongoza kupitia kwako kuhusu maudhui ya waraka uliotolewa na waheshimiwa maaskofu wa KKKT siku ya Jumamosi tarehe 24 Machi 2018. Waraka huo ulitarajiwa kusomwa katika makanisa siku ya Jumapili tarehe 25 Machi 2018. Katika kutoa maoni yangu kuhusu waraka huo, ninalenga mambo makubwa mawili ambayo ni pongezi kwenu, na pili ni mtazamo wangu juu ya baadhi ya masuala yaliyomo katika waraka huo.

Mheshimiwa Baba Askofu, kwa dhati kabisa ninawapongeza sana kwa kujali na kwa utayari wenu katika kuzungumzia na kuchambua kwa kina mambo muhimu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yanayogusa moja kwa moja uhai na haki za kibinadamu za waumini wa KKKT na Watanzania kwa ujumla.

Aidha, ninawapongeza sana kwa ujasiri na kwa kutumia vizuri nafasi zenu katika kanisa na jamii ya Watanzania katika kuyatolea kauli mambo yanayogusa masilahi mapana ya nchi yetu.

Kupitia waraka huo, mmetimiza ipasavyo majukumu yenu ya msingi kwa jamii. Binafsi ninaamini kuwa pamoja na kwamba ninyi ni viongozi wa kiroho, bado mnayo nafasi kubwa katika kuchangia maendeleo ya nchi yetu kisiasa, kijamii na kiuchumi kwani mambo yote hayo yana uhusiano wa moja kwa moja na afya ya kiroho.

Mheshimiwa Baba Askofu, mbali ya pongezi hizo, nina maoni kwenu ninyi viongozi wetu wa kiroho katika mambo kadhaa yaliyobainishwa kwenye waraka, ambayo ninaona kuwa maudhui yake hayaakisi hadhi na wajibu wa msingi wa kanisa.

Kama ambavyo mmekuwa mkitufundisha siku zote, na vile tusomavyo katika Biblia Takatifu, ninafahamu kuwa kazi za msingi za kanisa ni zile ambazo Bwana Yesu Kristo alizifanya alipokuwa duniani. Kazi hizo ni kuhubiri habari njema (injili), kufundisha waumini ambao ni sehemu ya jamii na kuponya wenye shida mbalimbali kijamii, kimwili na kiroho.

 Ninaamini kuwa ninyi viongozi wetu wa kanisa ni warithi wa kazi hizo wenye wajibu wa kuziendeleza hapa duniani. Inatarajiwa kuwa maneno na matendo yenu ndani na nje ya kanisa yatakuwa yenye mwelekeo wa kutekeleza kazi hizo ambazo matokeo yake ni uponyaji wa jamii na kuleta matumaini ya kimaisha, kiroho na kimwili.

Mheshimiwa Baba Askofu, katika waraka wenu mmetoa maoni katika maeneo 18 ambayo mmeyagawanya katika maeneo makuu matatu (jamii na uchumi; maisha ya siasa na masuala mtambuka). Kwa ujumla, ninakubaliana na mengi mliyogusia katika waraka huo na ninaamini yamefundisha na kuponya roho zetu kwa kiasi kikubwa, hasa kipingele cha tano (v) mnapozungumzia masula mtambuka pale mnaposema: “Uhai wa mtu una thamani isiyopimika. Ni wajibu usiokwepeka kuulinda na kuutunza uhai kwa vitendo halisi. Endapo uhai umepotea katika mazingira yoyote, uchunguzi huru na wa haki ufanyike na taarifa zitolewe kwa wakati muafaka ili kujenga jamii yenye imani kwa Serikali na vyombo vyake”.

Hata hivyo, yapo maeneo matano (5) muhimu mliyoyatolea kauli ambayo, kwa maoni yangu, hayaponyi bali yanaleta mkanganyiko zaidi kwa jamii kwa kuwa hayakujengwa katika msingi wa mantiki na ushahidi wa neno la Mungu, wala kuzingatia mantiki na ushahidi wa kisayansi, ambayo siku zote yamekuwa ni msingi wa hoja za KKKT.

Mheshimiwa Baba Askofu, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, naomba sasa niyabainishe maeneo hayo matano ambayo ninaamini kuwa mngejipa nafasi ya kutafakari kwa kina zaidi msingeyatolea kauli au mngeyatolea kauli kwa namna nyingine.

1.Kuhusu uhuru wa Bunge, Mahakama na Tume ya Uchaguzi
Mheshimiwa Baba Askofu, katika kujadili maisha ya siasa, katika hoja yenu ya nne (4), mmeeleza kwamba kuna “kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama na Tume ya Uchaguzi”.

Maoni haya siyo mageni na yamesambaa mtaani na hasa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani. Hata hivyo, maoni kama haya yanapotolewa na ninyi viongozi wetu wakuu wa kiroho yanakuwa na mwangwi tofauti katika jamii.

Suala hili la uhuru wa Bunge na Mahakama ni mjadala wa kudumu katika siasa duniani kote. Hii inatokana na ukweli kwamba hakuna kigezo kimoja kilichokubalika duniani kote cha kupima uhuru wa Bunge na Mahakama. Kila jamii au upande una tafsiri yake kutokana na muktadha wa nchi husika.

Mheshimiwa Baba Askofu, labda nifafanue hoja yangu kwa kutumia mfano wa Bunge. Katiba yetu ipo wazi kwamba Bunge ndicho chombo cha mamlaka ya juu (supreme) katika mihimili mitatu ya dola nchini mwetu.

Aidha, katika mfumo wa vyama vingi, Bunge huongozwa kwa msingi wa demokrasia ya wachache wasikilizwe lakini wengi waamue. Katika Bunge letu la sasa, idadi ya wabunge wa chama kinachounda Serikali yaani CCM, ni zaidi ya theluthi mbili ya idadi ya wabunge wote.

Hii inamaanisha kuwa, kwa mujibu wa Katiba yetu na sheria zake, kwa Bunge hili wabunge wa CCM ndiyo wenye haki ya maamuzi kutokana na idadi yao. Kwa sababu hii, kama kuna tatizo katika mfumo wa maamuzi wa Bunge letu, tatizo la msingi haliwezi kuwa kukosekana kwa uhuru wa Bunge kwa kuwa Katiba yetu imetoa uhuru wa kutosha kabisa kwa chombo hiki. Ingekuwa ni tatizo kama kuna siku Bunge lingekuwa limeamua kinyume cha matakwa na maamuzi ya walio wengi ndani ya Bunge.

2.Kuhusu wanasiasa kuhama vyama
Mheshimiwa Baba Askofu, eneo la pili ambalo nina maoni tofauti ni katika hoja yenu ya saba linalohusu maisha ya siasa. Katika eneo hili hoja yenu ya msingi ni kwamba kuna udhalilishaji wa kauli njema isemayo “maendeleo hayana chama”. Waheshimiwa Maaskofu mnadai kuwa “udhalilishaji huu unafanyika kwa njia ya kutumia fedha nyingi katika chaguzi ndogo zinazotokana na watu wanaobadili vyama ili kuleta maendeleo”. Mmeendelea kujenga hoja kwa kujiuliza, “kama maendeleo hayana chama, kwa nini mtu anajiuzulu chama fulani eti kwenda kingine?”

Mheshimiwa Baba Askofu, katika utangulizi wa waraka wenu, mmeeleza vizuri sana kuhusu umuhimu wa kudumisha mfumo wa vyama vingi. Hata hivyo, kwa maoni yangu, kauli yenu niliyoinukuu hapo juu haikuzingatia ipasavyo utamaduni unaoambatana na mfumo wa vyama vingi.

Duniani kote, pamoja na mambo mengine, utamaduni wa mfumo wa vyama vingi huambatana na watu kuhama vyama kila wanapojisikia kufanya hivyo. Vyama vya siasa ni taasisi ambazo wanachama wake wapo huru kuingia na kutoka bila kutakiwa kujieleza kwa mtu yeyote yule ilimradi katika kufanya hivyo hawavunji sheria za nchi.

Labda nikupeni mifano michache katika kupanua uelewa wa jambo hili. Katika nchi ya jirani Kenya viongozi wote wakuu katika siasa za Kenya wamewahi kuhama vyama mara nyingi. Rais wa sasa wa Kenya ameshahama na kubadili vyama mara nne. Kiongozi nguli wa upinzani Raila Odinga ameshahama na kubadilisha vyama mara sita. Huko nchini Uganda kiongozi maarufu wa upinzani nchini humo Kiiza Besigye alikuwa katika chama kimoja na Rais Museveni, lakini alihama na kuanzisha chama chake.

Pengine unaweza ukasema tabia za kuhama vyama zipo Afrika tu. Hapana. Muasisi wa kuhama vyama duniani ni Winston Churchil, ambaye ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa waziri mkuu bora nchini Uingereza. Huyu alihama kutoka chama cha Conservative na kujiunga na chama cha Liberal. Baadaye tena alirudi katika chama cha Conservative na hatimaye kuchaguliwa kuwa waziri mkuu.

Ukienda nchini Marekani wapo wanasiasa maarufu 21 waliowahi kuhama vyama vyao. Kwa mfano, rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alikuwa mwanachama wa chama cha Democrat, lakini alihamia chama cha Republican na baadaye akaja kuwa rais wa nchi hiyo.

Alipoulizwa kwa nini alihama alijibu kuwa “I didnt leave the Democratic Party. The party left me” (Sikukiacha Chama cha Democrat. Chama ndicho kilichoniacha). Wanasiasa wengine maarufu waliowahi kuhama vyama vyao nchini Marekani ni pamoja na Condoleeza Rice, Elizabeth Warren, Hillary Clinton na Theodore Roosevelt. Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump alishahama vyama mara tatu na hadi mwaka 2001 alikuwa mwanachama wa chama cha Democrat.

Mheshimiwa Baba Askofu, nimetoa mifano yote hii katika kujaribu kupanua uelewa wenu kuhusu tabia za wanasiasa katika mfumo wa vyama vingi duniani kote. Hata hivyo, jambo hili halipo katika siasa tu. Wewe unafahamu vizuri kuwa hata katika dini watu hubadili dini na madhehebu yao. Sembuse vyama vya siasa?

Aidha, katika nchi yetu tumeshakuwa na chaguzi ndogo nyingi zinazotokana na wabunge na madiwani ama kuhama vyama vyao au kufukuzwa katika vyama vyao tangu mfumo wa vyama ulipoanza, na chaguzi zote hizo husababisha gharama kubwa. Sasa ninajiuliza kwa nini Kanisa limeumia sana na chaguzi za kipindi hiki? Kuna nini?

3.Kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu
Mheshimiwa Baba Askofu, hoja ya tatu ambayo nayo pia ningependa kuitolea maoni ipo katika eneo la tatu la waraka wenu, ambayo ni kuhusu upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu. Katika hoja hiyo mmeeleza kwamba, “uwezeshwaji wa vijana kupata mikopo ya elimu ya juu uwe shirikishi na usiokuwa na ubaguzi kati ya wanafunzi wa vyuo binafsi na wale wa serikali; sayansi na sanaa; wazazi maskini na wenye nafasi; waliosoma shule binafsi na wale wa shule za Serikali”.

Kwa ufahamu wangu ni kwamba kimsingi kila mkopo lazima uwe na vigezo. Msingi mkubwa wa mikopo inayotolewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini ni kile kinachofahamika kama means testing, ambapo Bodi ya Mikopo huchambua maombi ya mikopo kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, uwezo wa wazazi wa wanafunzi. Hivyo, mnaposema pasiwe na tofauti katika utoaji wa mikopo, mlitaka kumaanisha nini hasa?

Ni vizuri kukumbushana kuwa kuanzishwa kwa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kulitokana na Serikali kushindwa kugharamia wanafunzi wote wanaodahiliwa katika elimu ya juu. Kwa sababu hii, njia pekee ilikuwa ni kuja na vigezo ambavyo vingewaondoa wale ambao wana uwezo wa kujilipia.

Katika mazingira haya, sio sahihi, kwa mfano, kusema kuwa hata mtoto wa mzazi mwenye wadhifa kama wangu naye apate mkopo. Aidha, kanisa haliwezi kueleweka linapotaka mtoto aliyesomeshwa na mzazi wake katika Shule ya Sekondari Feza au International School of Tanganyika naye apate mkopo wa serikali.

Aidha, kila nchi duniani ina vipaumbele vyake vya mahitaji kutokana na wakati na mazingira. Kwa wakati na mazingira ya nchi yetu kwa sasa tunahitaji zaidi wataalamu katika fani za sayansi kuliko sanaa.

Ni kwa sababu hii Serikali inawekeza zaidi katika kusomesha wanafunzi katika fani za sayansi kuliko sanaa. Huu ndiyo msingi wa Serikali kuwapa kipaumbele wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kuliko wale wanaosoma masomo ya sanaa.

Kwa maoni yangu, jukumu la kanisa katika suala hili lingekuwa ni kuiasa serikali kuepuka ubaguzi katika mikopo kwa misingi ya dini, itikadi za siasa na ukabila ambapo bahati nzuri ubaguzi huo haupo.

Ubaguzi katika mikopo ya elimu ya juu kwa misingi ya uwezo wa wazazi na aina ya shule ambayo mtoto alisoma (binafsi au umma) hauepukiki. Kwa maoni yangu, kuna haja pia kuangalia kama bado ni muhimu kutoa kipaumbele kilicho sawa kati ya wanafunzi wanaodahiliwa katika vyuo vikuu vya umma na wale wanaodahiliwa katika vyuo vikuu vya binafsi.

Huo pia unaweza ukawa aina nyingine ya ubaguzi unaokubalika katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, hasa katika mazingira ambayo vyuo vya umma vina nafasi ya kutosha ya kudahili wanafunzi wote wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu.

4.Katiba Mpya
Mheshimiwa Baba Askofu, katika waraka wenu mmetoa pia maoni kuhusu umuhimu na uharaka wa kupatikana kwa Katiba mpya. Hii ni hoja kubwa inayogusa Taifa letu kwa muda mrefu. Sote tunatambua utashi na ujasiri aliouonyesha Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne wa kuruhusu mchakato huu uanze, pamoja na kwamba haikuwa ajenda ya msingi na kipaumbele katika chama chake. Kwa hiyo, ninaunga mkono kanisa kulitolea kauli jambo hili kubwa na muhimu kwa Taifa letu.

Hata hivyo, baadhi ya hoja zenu na lugha iliyotumika katika kuwakilisha hoja hiyo haiponyi bali inaligawa kanisa na nchi kwa ujumla. Kwa mfano, mnaposema kuwa “tunaisihi Serikali ya Awamu ya Tano kurejea mchakato wa upatikanaji wa KATIBA MPYA ya wananchi iliyopendekezwa na wananchi kupitia Tume ya Warioba”, mlitaka kumaanisha nini hasa?

Ninauliza hivi kwa sababu ninafahamu kuwa mchakato wa kuunda Katiba mpya ulikuwa umevuka ngazi ya Tume ya Warioba na kufikia ngazi ya Bunge la Katiba, ambapo Bunge lilipitisha kwa kura ya wengi.

Kilichokwama katika mchakato huo ni kura ya maoni ya wananchi kutokana na kukosekana kwa maridhiano mapana ya kijamii baada ya baadhi ya wawakilishi katika Bunge la Katiba kususa kuhudhuria vikao vya Bunge hilo.

Ninafahamu pia kuwa kanisa na dini zingine ziliwakilishwa kikamilifu katika Bunge hilo. Wawakilishi wa kanisa sio miongoni mwa wabunge waliosusia Bunge la Katiba, ikimaanisha kuwa kanisa liliridhia mchakato hadi mwisho na ni sehemu ya jamii waliokubaliana na rasimu iliyopitishwa na Bunge hilo.

Sababu za msingi za mchakato wa Katiba kukwama ni kutokana na kukosekana kwa mwafaka na maridhiano ya kitaifa. Kwa sababu hii mchakato wa Katiba mpya umebaki ukielea. Sasa katika mazingira haya ni hatari sana kwa ninyi viongozi wetu wakuu wa kiroho kuchukua upande mmojawapo katika mgawanyiko huo uliotokea.

Kwa maoni yangu, kwa upande wenu kama kanisa ingetosha kutoa wito wa kurejewa kwa mchakato wa Katiba mpya na kutoa wito wa mchakato huo kuzingatia maridhiano ya kitaifa.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa Sauti za Wananchi yaliyotolewa mwezi Oktoba 2017, maoni ya wananchi yamegawanyika katika makundi manne kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya. Kuna kundi la Watanzania linalotaka mchakato uanze upya. Kuna kundi jingine linalotaka turejee kwa Tume ya Warioba.

Lipo kundi linalotaka tumalizie mchakato kwa kwenda katika kura ya maoni. Lakini pia wapo Watanzania wanaosema hakuna haja tena ya Katiba mpya. Makundi yote haya ni ya Watanzania na bila shaka miongoni mwao ni waumini wa KKKT. Hivyo, ninyi viongozi wetu mnapoongelea suala hili kwa namna ya kuhimitisha (conclusive) mnajiweka katika mazingira ya kuchochea mgawanyiko badala ya kuleta umoja na uponyaji.

5.Kuhusu Serikali kutoendeshwa kwa ilani ya vyama
Hoja yenu nyingine katika eneo la maisha ya siasa ni kuhusu nafasi ya ilani ya vyama katika kuendesha nchi na Serikali. Katika hoja yenu hii mmenena ya kuwa, “Taifa haliongozwi na ilani za vyama. Serikali haiongozwi na ilani za vyama. Serikali huongozwa na Katiba, sheria, kanuni na mapokeo mema (misingi na tunu za Taifa)”.

Baba Askofu, niruhusu nikupeni elimu ya siasa kidogo kuhusu jambo hili. Duniani kote inajulikana kuwa chama kinachopata ridhaa ya kuunda serikali hupewa dhamana ya kutekeleza ahadi ambazo chama hicho kilizitoa katika uchaguzi.

Ndiyo kusema, vyama vinapoingia kushindana katika uchaguzi hushindania fursa ya kuunda serikali ili vitekeleze yale ambayo vinaamini ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa husika. Kwa hivyo, msingi wa sera za serikali iliyopo madarakani ni ilani ya chama tawala iliyosheheni ahadi za chama hicho wakati wa uchaguzi.

Ndiyo kusema mara chama kinaposhinda uchaguzi na kuunda serikali ahadi zake zilizopo ndani ya ilani hugeuka kuwa ajenda za maendeleo za Taifa hilo. Ndiyo maana ahadi za CCM za uchaguzi wa mwaka 2015 ni sehemu muhimu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.

Kwa hiyo serikali huongozwa na vyombo vikubwa viwili katika kuendesha nchi. Chombo cha kwanza ni ilani ya chama tawala ambayo hutekelezwa kama sehemu ya ajenda za maendeleo ya Taifa husika.

Chombo cha pili ni Katiba, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ambayo hutolewa na vyombo mbalimbali vya dola. Katiba, sheria na kanuni ni nyenzo za utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa, ikiwemo ilani ya chama tawala.

Hadi hapo utaona kuwa hamkuwa sahihi hata kidogo kuwahubiria waumini wa KKKT na Watanzania kwa ujumla kuwa Serikali haiendeshwi kwa ilani za vyama. Ukweli ni kuwa ilani ya chama tawala ni nyenzo na ajenda muhimu ya kuendesha serikali katika nchi zote zinaendeshwa kidemokrasia na kwa kufuata utawala wa sheria.

Marekani, kwa mfano, leo wanajenga ukuta wa kuitenga Marekani na Mexico ili kudhibiti wahamiaji kutoka Mexico. Hii ilikuwa ni moja ya ahadi kubwa za Rais Donald Trump na chama chake cha Republican wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2016. Baada ya Donald Trump kushinda uchaguzi na kuunda serikali ahadi hii sasa ni ajenda ya Taifa la Marekani.

Mheshimiwa Baba Askofu, nihitimishe barua yangu kwa kurudia tena pongezi za dhati kwa kuandaa Waraka ambao umegusa masuala nyeti yanayohusu nchi yetu. Hata hivyo, upo umuhimu kwa kanisa kujiepusha kadri inavyowezekana kuonekana lipo upande fulani kwenye mijadala ya kitaifa inayogusa jamii pana yenye mitazamo kinzani.

Kwa kufanya hivyo, mtaepusha migawanyiko isiyo ya lazima kwa waumini ndani ya kanisa na wananchi kwa ujumla. Ushauri wangu ni kwamba ili kanisa lionekane linaendeleza kazi za msingi zilizoanzishwa na Bwana wetu Yesu Kristo, ni muhimu sana kufanya utafiti na uchambuzi wa kina wa jambo lolote kabla ya kulitolea kauli hadharani.

Aidha, ni muhimu kwa kanisa kupima kwa umakini mkubwa uzito wa kila neno kabla ya kutoa kauli katika umma. Ni hatari kwa kanisa kutoa kauli inayosababisha maumivu na mifarakano badala ya kuponya. Ili kuepuka kauli za namna hii, ni vizuri kila mara kanisa na viongozi wetu mkajenga hoja zenu kwa kuzingatia mantiki na ushahidi wa kiinjili unaopatikana ndani ya Biblia Takatifu, na/au mantiki na ushahidi wa kisayansi unaopatikana kupitia tafiti na tafakuri pana na shirikishi.

Mheshimiwa Baba Askofu, Bwana Yesu Asifiwe.
Kwa heshima na taadhima ninaomba kuwasilisha.
Dodoma
Alhamisi 29 Machi 2018.

Friday 16 March 2018

BAADA YA KUITOA AC MILAN EUROPA LEAGUE, WENGER AHOFIA KUKUTANA NA ATLETICO, KAYASEMA HAYA



Baada ya Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AC MIlan usiku wa jana kwenye hatua ya 16 ya Europa League, Kocha Arsene Wenger amesema hahitaji kukutana na Atletico Madrid.

Atletico na Arsenal zimefuzu kuingia hatua ya nane bora ya michuano hiyo huku droo ya timu zitakazokutana robo fainali ikitaraji kufanyika kesho.

Wenger amesema anatamani kutokupangwa na timu hiyo ya Spain ili aweze kupata unafuu wa kupenya kwenye mashindano hayo.

Aidha Wenger amesema kuwa wamekutana na wakati mgumu katika mechi zilizopita hivi karibuni na hatimaye wamekuja kupata matokeo kwenye michezo ya mwisho.

Arsenal imefuzu kuingia hatua hiyo baada ya kuifunga AC Milan kwa jumla ya mabao 5-1.

Tuesday 13 March 2018

Wasichana Wahimizwa Kupima Kubaini Maumbile ya Uke ni ya Kawaida


Wasichana nchini Uingereza wanahimizwa kutumia huduma ya mtandaoni ili kuwasaidia kuangalia iwapo maumbile ya uke wao ni ya kawaida.

Huduma hiyo inapatikana kwenye mtandao wa masuala ya afya ya uzazi na ngono wa Brook, ambao unatoa mifano kwa kutumia video na kutoa ushauri kuhusu jinsi sehemu za siri za mwanamke hubadilika wakati anapobalehe au kuvunja ungo.


Watafiti wa afya waliotengeneza mtandao huo wamesema wana matumaini kwamba wasichana wataanza kujiamini zaidi na kuwafanya kutotaka ''upasuaji wa urembo'' wa sehemu zao siri.

Upasuaji wa aina hiyo haustahili kufanyiwa kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 18.


Upasuaji huo wa urembo wa sehemu nyeti maarufu kama- labiaplasty - unaofanywa kuongeza au kupunguza sehemu hizo hutekelezwa na madaktari binafsi ambao hutoza maelfu ya mapauni.

Kwa mara nyingi, operesheni hiyo huweza kufanywa na mamlaka ya huduma ya afya -NHS iwapo sehemu nyeti za msichana zina kasoro, iwapo inamsumbua au inamwathiri kiafya.

Madaktari wa afya hawastahili kutoa uamuzi kwamba wasichana wafanyiwe upasuaji kwa sababu ya urembo pekee.

Kulingana na takwimu za NHS, 2015-16 zaidi ya wasichana 200 chini ya miaka 18 walifanyiwa upasuaji wa sehemu zao za siri na zaidi ya 150 ya wasichana hao walikuwa chini ya miaka 15.

Bi Louise Williams, ambaye ni muuguzi katika chuo kikuu cha University College Hospital na kiongozi wa mradi huu, amesema: "Elimu hii itawasaidia wasichana kuelewa sehemu zao za siri na jinsi inavyokomaa wakati wanapovunja ungo, haswa wakiwa na wasiwasi jinsi wanavyojitizama au kijihisi.

"Tuna matumaini kwamba tutawahakikishia wasichana kwamba sehemu zao za siri ziko na maumbo tofauti na ukubwa fulani na iwapo wanahitaji usaidizi na mawaidha , wanaweza kujua pale watakapopata ujumbe huu.''

Dkt Naomi Crouch kutoka chuo cha taasisi cha Royal College cha Madaktari wa uzazi na wataalamu wa afya ya uzazi na shirika la Uingereza la watoto pia walihusika kwenye utafiti huo.

Wasichana wadogo Uingereza wafanyiwa upasuaji uke wao
Mwanamume atolewa uvimbe wa kilo 1.8 India
Alisema: "Hakuna utafiti wowote wa kisayansi ambao unaounga mkono upasuaji wa sehemu za siri na iwapo una athari zozote za kimwili au kisaikolojia hasa kwa vijana ambao bado wanakuwa.

"Tunatumai kwamba ujumbe huu utawapatia wasichana ufahamu zaidi kwa kwamba sehemu zao za siri ni maalumu na hubadilika wanapokua maishani na ni kawaida."

Sunday 11 March 2018

Tarehe / Siku Nzuri kwa Mimba Kuweza Kutungwa


Leo napenda nizungumzie jambo moja tu ambalo ni juu ya  jambo moja tu, nalo ni namna wanavyoweza kui-pin point siku ile ya kilele (i.e fruitful/productive/fertile day), hapa nina maana ya siku ile ambayo wao wanaiita siku ya 14.

Ikumbukwe kuwa wanawake wanatofautiana katika suala zima la urefu wa MENSTRAL CYCLE, yaani idadi ya siku kati ya period ya kwanza hadi ile ya pili inayofuatia. Kundi kubwa la wanawake wana fall kwenye range ya siku 22-35. Japo walio-normal wana siku 28. Vile vile kuna wengine huwa na menstral cycle mbili, yaani fupi na ndefu. Hivyo walio na menstral cycle fupi, mathalani wale wenye siku 22, huwa vilevile wana kipindi kifupi sana cha kutokwa na damu (period), yaani damu inaweza kukatika ndani ya siku 2 tu! Na wale wenye siku 35 au zaidi huwa wana kipindi kirefu sana cha kutokwa na damu (period) ambapo wengine huwachukua hata siku kati ya 5 hadi 8.

Hivo basi, kama wewe ni mwanaume inakubidi umwelewe vizuri mwenzi wako juu ya hayo niliyoyasema hapo juu ili ikusaidie kui-pin point ile fertile day (yaani siku ya mimba).

Swali: Je siku ya mimba ni ipi?
Jibu lisilosahihi: Watu wengi na hata baadhi ya wanasayansi wanafikiri siku ya mimba ni ile ya 14 baada  ya dalili za kwanza za damu ya hedhi! Wao huhesabu kuanzia siku ile damu ilipoanza kutoka hadi siku ya 14! Utaratibu huu ume-prove failure! Hii ni kwa sababu wanawake wana menstral cycle
zinazotofautiana kwa urefu. Hivo basi jibu sahihi ni hili hapa chini:

Jibu sahihi: 
1. Kwanza inabidi ujue kama mwenzi wako ana menstral cycle ipi? Fupi au ndefu, ama zote mbili?

2. Baada ya kujua urefu wa menstral cycle ya mwenzi wako then pin point siku ile ya mwisho halafu
uhesabu backwards siku 15 kuanzia siku ile ya mwisho. Siku hii ya 15 kuanzia mwisho ndiyo siku ya  mimba kwa mwanamke yeyote!

Once you know the '15th day' from the last one, then you can manoeuvre whatever you want to get her pregnant or to avoid pregnancy!

With this new approach of pin pointing the fertile day you will find that all women (menstral cycles)
are covered, whereas the old way of counting fits only to women whose menstral cycles are 28 days!


Naomba nitoe mifano hai kwa faida ya dada zetu na wengine:
1. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa
chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th,
20th, 21st, 22nd.

Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya
kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake. Hivo 8th day ndiyo siku ya mimba
kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22. Akumbuke kwamba 1st day
ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


2. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa
chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th,
20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya
kumi na tano inaangukia kwenye 14th day. Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba
kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 28. Akumbuke kwamba 1st day
ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


3. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa
chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th,
20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya
kumi na tano inaangukia kwenye 21st day. Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa
mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 35. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo
siku anayoanza ku-bleed!


4. Kama mwanamke ana abnormal menstration cycle ya siku 15 , BASI KUNAUWEZEKANO
WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama
kawaida:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya
kumi na tano inaangukia kwenye 1st day. Inamaana kwamba, the 1st day of her bleedind ndiyo
siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 15. Akumbuke
kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa
kundi hili anaweza kupata mimba!

Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo
ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa. Mwanamke wa aina hii
anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku
ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili
linakuwa tayari kurutubishwa!

Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa
kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu
kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed. Pia wanawake wa kundi hili huwa
wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu; na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

Jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hawana knowledge ya kutosha juu ya hili
suala la siku ya mimba; hasa wale ambao wana menstration cycle inayobadilikabadilika! Wao
husitukia tu wameanza ku-bleed. Ndo maana hawawezi hata ku-plan kutopata mimba! Hawana
ujanja kabisa ndio sababu wengi wanatumia sindano na njia zingine nyingi za artificial ambazo
mwisho wa siku huwaletea matatizo ya uzazi, kwani nyingi hu-block njia ya uzazi! Nimeona
wengi wenye matatizo ya uzazi unaosababishwa na hizi artificial family planning. Wengine
hulazimika kwenda hospital kuzibuliwa ili wapate mimba jambo ambalo ni hatari kwa afya zao!
Full maelezo ya kujitosheleza, ukikosa kudaka au kudakisha mimba basi kuna walakini...

Maandamano Yamwibua John Cheyo....Ataka Mabaraza ya Vyama Yatumika Badala ya Watu Kuandamana



Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo amesema mabaraza ya vyama vya siasa yakitumika kikamilifu yanaweza kuondoa malalamiko ya wananchi na viongozi wa upinzani.

Amesema hayo leo Machi 11,2018 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu vuguvugu la maandamano yaliyopangwa kufanyika Aprili 26,2018 yanayoratibiwa kupitia mitandao ya kijamii.

Cheyo amesema maandamano hayo ni uchochezi na uvunjifu wa amani na kwamba, mambo yanayolalamikiwa yangeweza kutatuliwa kupitia mabaraza hayo.

"Tusitake kufika hatua ya kuandamana barabarani ili kudai haki, Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi. Tukifikia huko amani iliyopo Tanzania tutashindwa kuipata tena na wananchi watakosa nchi nyingine yenye amani ya kukimbilia," amesema.

Cheyo amesema kama tatizo ni fedha kwa ajili ya mabaraza hayo kukutana, Rais John Magufuli anapaswa kutoa fedha kuyawezesha kufanya vikao.

"Siungi mkono hoja za kudai kuwepo mikutano ya hadhara hata kama ni kwa ajili ya kuongeza wanachama kama wanavyodai wengine, naamini kwa sasa mitando ya kijamii ina nguvu kuliko kitu chochote nchini," amesema Cheyo.

Amesema kabla ya kudai haki ya kuandamana, zipo nyingine wananchi wapaswa kuzipa kipaumbele zikiwemo haki ya kuishi, kupata maji safi na salama, elimu na afya.

"Hatuwezi kufika mahali tuseme nchi hii imepotea na hakuna demokrasia kisa tumekosa haki ya kuandamana, haki ya kufanya mikutano ya hadhara. Kila mtu alishuhudia mikutano ya kampeni za uchaguzi wa ubunge wa marudio katika majimbo ya Kinondoni na Siha ilivyogeuka sehemu ya kutukanana," amesema Cheyo.

"Kama kitu mnachokidai kiliweza kusababisha watu kugombana na askari hadi mauaji yakatokea hicho kitu hakitusaidii kama nchi," amesema.

Cheyo amesema yanayodaiwa kwa nguvu hayana faida na manufaa ya kila siku kwa sababu watu wanahitaji kupata wakati wa kulima na kuvuna.

"Hiyo mikutano iliyoshupaliwa sasa na kuhitajika kwa nguvu zote si kweli kwamba kila siku watakuwa barabarani kuhutubia wananchi, fedha tutatafuta saa ngapi, tutalima saa ngapi, hivyo ni vyema tutambue kila kitu kinachofanyika kupitia mambo ya siasa kisiwe kisingizio cha kusema nchi haina amani, haina uhuru," amesema Cheyo.

Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwa kiunganishi cha wananchi na viongozi wa vyama vya siasa na si kufanya kinyume cha hilo.

Mwigulu aonya atakayeandamana ‘hata kuzunguka kitanda’


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu wote ambao wamepanga njama za kutaka kuwauwa watanzania katika maandamano ambayo wameyapanga kuyafanya

Mwigulu ametoa hiyo wakati alipokuwa akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli aliyopo Mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ambapo leo hii (Machi 11, 2018) amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika maandamano hayo ni namna ya watu wanatawanywa ili kusudi waje kulalamika kuwa serikali ndio imeuwa watu wake.

"Njama hiyo tumeiona na mimi nimemuelekeza IGP Sirro kwamba hata kupanga njama ya kuua ni kosa, wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi yetu ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma. 

"Watu wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu  ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa", amesema Mwigulu.

Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema "Mhe. Rais ndio maana unaona vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa.

"Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?, watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo, si jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano wala hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana".

Aidha, Waziri Mwigulu amesema endapo ikatokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba zao bado sheria itachukua mkondo wake dhidi ya watu hao.

"Ikitokea hata watu wakaandamana ndani ya nyumba wakazunguka kitanda na akatokea mtu akaumia, yule aliyeitisha waandamane pale atawajibika kwasababu watu wanafanya mzaha na maisha na dira ya nchi yetu ambapo Rais umejitoa muhanga kwa ajili ya kutengeneza urithi wa watoto wa Tanzania", amesisitiza Mwigulu.

Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu amesema yeyote atakayethubutu kutaka kuharibu taifa la Tanzania kwa kufanya vitendo vya uovu hawatoweza kumuacha salama.

Thursday 8 March 2018

Waziri akiri Kenya imekumbwa na upungufu mkubwa wa fedha


Wizara ya fedha nchini imekiri kwa serikali inakumbwa na changamoto kubwa za kifedha na haiwezi kabisa kutimiza mahitaji yake.

Ufadhili wa miradi muhimu ya serikali umeathiriwa zikiwemo serikali za kaunti ambazo bajeti zao, serikali itazipunguza kwa shilingi bilioni 15 na 17 au dola [147,913,193 na 167,634,953].

Kutokana na ukosefu huo wa fedha mashirika ya serikali yametakiwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kutumia fedha zilizopo kwa njia inayostahili.

"Kila shirika ni lazima lijizatiti. Tumebuni njia ya kupunguza matumizi. Tunapunguza matumizi kwa kila sekta ili kwenda sambamba na fedha zetu," alisema waziri wa fedha Henry Rotich.

Amesema kuwa hali hii imetokana na kushindwa kwa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya KRA kushindwa kutimiza malengo yake yote ya kukusanya ushuru na kipindi kirefu cha shughuli za uchaguzi.

"Tumeongea na KRA Jinsi tunaweza kukabiliana na hilo kupitia ukusanyaji wa kodi ya ndani na ya nje," Rotich aliiambia Kamati ya ya seneti.

Kulingana na Rotich serikali inakabiliwa na upungufu wa ukusanyaji ushuru wa bilioni 70 kwenye makadirio ya serikali ya mwaka 2017/2018.

Kutokana hilo, kuna uwezekano kuwa wakenya watakumbwa na nyakati ngumu kwa sababu serikali itaendelea kukopa ndani ikishindana na watu, hali ambayo itachangia biashara ndogo kuwa na ugumu wa kupata mikopo kutoka kwa benki.

Hadi Disemba mwaka 2017 deni la Kenya lilikuwa shilingi trilioni 4.55, deni ambalo limesababisha nchi kutenga asilimia 54 ya pato lake kulipa madeni.

Maseneta walitaka kujua ni kwa nini serikali za kaunti hazijapokea fedha kwa miezi minne licha ya seneti kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo.

Alijibu na kusema kuwa ni shilingi bilioni 134 tu zimetolewa kwa serikali za kaunti kinyume na fedha zilizokuwa zikihitajika dola bilioni 302.

Enyi Wanaume Ishini na Wake Zenu Kwa AKILI" La Sivyo Mwanamke Atakukoroga Maisha Yako Yote



BIBLIA ILIPOSEMA "Enyi Wanaume Ishini na wake zenu kwa AKILI" Mungu alikuwa anajua anachosema.Kama huna akili Mwanamke atakukoroga maisha yako yote na utaishia kusema "Women are so Complicated"

Wanawake huwa wanaongea vitu 'Kirahisi-rahisi tu' lakini huwa vinamaanisha 'Vitu Vigumu Ajabu'
Wanawake wanaweza kukwambia "Mi nataka Mwanaume anipende tu BHAASSS!!Ukidhani kwamba Upendo wako unatosha kwake UTAKUWA UMEFELI
Wanawake wanahitaji vitu 4 na vyote VIENDE KWA PAMOJA(Perpendicularly),vitu hivyo ni

1.HELA
2.GOOD S3X
3.CARING MAN
4.MUDA

Kuna Wanaume wanajua "Kukaza vizuri" mwanamke anatosheka,na wana hela ila WAKO BUSY...Hii factor ya wewe kuwa Busy tu itamfanya mtu mwingine mwenye Muda "Amkaze kiulaini kabisa" halafu wewe utashangaa..."Mke wangu nampa kila kitu,hela za kila kitu nampa..YES,Amekaa muda mrefu uko bize unasaka hela na adui namba 1 wa Mwanamke ni LONELINESS....

A lonely Woman can easily be trapped by anyone..hata Houseboy akimpa ATTENTION endlessly anakula mzigo

Unataka Mwanamke awe wako peke yako???Fuata kanuni ya KIBIBLIA, ishi nae kwa akili....Mpe MUDA..Mpe HELA...Mpe Kisago kitandani...Mpe CARE na ATTENTION
Sikiliza maneno ya Nabii Seth uyatendee kazi,maana TB JOSHUA hatakwambia haya KAMWE!Nimemaliza!

Source:Nabii Seth

Monday 5 March 2018

ACT Wazalendo: Diwani atakayehama chama atatengwa na jamii


Katibu wa chama cha ACT - Wazalendo Jimbo la Kigoma mjini, Azizi Ally ametoa onyo kali kwa madiwani wa chama hicho kuwa atakayekihama na kujiunga CCM atatengwa na jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Machi 5, 2018 mjini hapa kufuatia kuwepo taarifa ya madiwani wanne kupanga mikakati ya kukihama chama hicho na kujiunga CCM.

Ally amebainisha kuwa diwani yeyote atakayehamia CCM atakuwa amejimaliza kisiasa kwani jamii nzima ya watu wa Kigoma itamtenga na kamwe asitarajie kushinda tena udiwani katika kata yoyote.

"Tulifanya kazi kubwa kuhakikisha wanashinda udiwani mwaka 2015, tukatumia gharama kubwa ya fedha za kampeni na muda wetu. Kamwe chama hakitakuwa tayari kuona diwani wake akihamia CCM,"amesema Azizi.

Ili kuwadhibiti madiwani hao, amesema wote waliitwa katika kikao maalumu cha chama na kuhojiwa juu ya kuwepo taarifa ya kukisaliti chama chao na kujiunga CCM, jambo ambalo walikanusha.

"Tumekaa na wazee wa chama chetu na madiwani wote wamedai wapo tayari kupigania chama, isipokuwa mmoja ndio hakuwepo," amesema.

Kwa upande wake, katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma, Naomi Kapambala ametamba kwamba kuna madiwani wa upinzani watajiunga na CCM wakati huu wa ziara ya katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphey Polepole.

ACT wana madiwani 19 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo CCM ina madiwani wanane na Chadema mmoja.

Waziri Charles Tizeba kuwa mgeni rasmi mechi ya Simba v Al Masry


Klabu ya Simba imetangaza kutarajia ugeni rasmi wa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry SC kutoka Egypt.

Simba itamkaribisha Tizeba kuongoza maelfu ya mashabiki wataoenda kuipa hamasa timu yao Uwanjani kwenye mechi hiyo itakayowakilisha taifa kwa ujumla.

Simba itakuwa inacheza na Al Masry baada ya kusonga mbele katika mashindano hayo, kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Gandermarie Nationale FC ya Djibout.

Mchezo huo utachezwa saa 12 jioni katika Uwanja wa Taifa dar es Salaam siku ya Jumatano wiki hii.

Afrika Kusini: Shirika lataka ukweli kuhusu mauaji ya mwanafunzi Mtanzania Baraka Naferi


Wanachama wa Shirika la Africa Diaspora Forum wamefanya mandamano nchini Afrika Kusini kushinikiza serikali ya nchi hiyo na serikali ya Tanzania kubaini ukweli kuhusu kuuawa kwa mwanafunzi raia wa Tanzania mwezi jana.

Bw Baraka Leonard Naferi, mwanafunzi wa shahada ya uzamifu, alifariki baada ya kugongwa na gari la teksi nje ya bweni la chuo kikuu.

Maafisa wa shirika hilo wameandamana kwa pamoja nabaadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Johannesburg nje ya bweni kwa jina Sophiatown ambapo mwanafunzi huyo alikuwa anaishi.

Mshukiwa alikamatwa na polisi wa Afrika Kusini lakini baadaye akaachiliwa huru kwa dhamana.

Polisi walisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka ya mauaji.

Badala yake, Mwandishi wetu Omar Mutasa aliyeko Johannesburg anasema polisi walimfungulia mashtaka ya kuendesha gari bila leseni.

Waandamanaji wameweka shada la maua kwenye uzio wa bweni la Sophiatown alipouawa Bw Baraka.

Bw Baraka aliuawa mnamo 23 Februari.

Baadhi ya wanafunzi wanasema kuna kanda ya video za usalama ambayo inamuonesha mwanafunzi huyo akikimbia na mwanafunzi mwingine, nyuma wakiandamwa na watu wawili waliokuwa ndani ya gari la teksi.

Gari hilo linaonekana kuwakimbiza na hatimaye Baraka anagongwa mara kadha akiwa kwenye uzio wa bweni.

Bashe afunguka haya


Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia matukio mbalimbali yanayojitokeza katika ardhi ya Tanzania na mwisho ameamua kuandika barua yenye hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ili kuundwe kamati ya teule ya uchunguzi.

Bashe ametoa kauli hiyo dakika chache zilizopita kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii na kuungwa mkono na wananchi kupitia 'comment' kwa uamuzi huo aliouchukua huku baadhi ya viongozi wa upinzani wakimpinga na kumuita mnafki kwa anachotaka kukifanya.

"Leo asubuhi nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kuunda Kamati teule ya Bunge kuchunguza matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa letu", amesema Bashe.

Kwa upande mwingine,  alipotafutwa Mbunge huyo kupitia simu yake ya kiganjani akadai hawezi kuliweka wazi suala hilo kwa sasa kwa maana amepanga kuzungumza na vyombo vya habari siku ya Alhamisi (Machi 8, 2018) ambapo ataweka bayana kuhusiana na mambo yanayotishia usalama na mshikamano wa taifa la Tanzania.

Kim Jong-un akutana na ujumbe kutoka Korea Kusini


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anaandaa mkutano wa chakula cha jioni na wajumbe wawili kutoka Korea Kusini, ikiwa ndiyo mara ya kwanza kiongozi huyo anakutana na ujumbe kutoka Kusini tangu aingie madarakani mwaka 2011.

Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap, liliripoti kuhusu mkutano huo likimnukuu msemaji wa rais nchini Korea Kusini.

Ujumbe huo uko nchini Korea Kaskazini kwa mazungumzo yasiyo ya kawaida yenye lenngo la kuanzisha mchakato kati ya Korea Kaskazini na Marekani.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeboreka kufuata mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi.

Ujumbe huo unawajumuisha maafisa wenye vyeo vya mawaziri - mkuu wa ujasusi Suh Hoon na mshauri wa usalama wa taifa Chung Eui-yong.

Awali Bw Chung aliwaambia waandishi wa habari kuwa atawasilisha azimio la Rais Moon Jae-in la kudumisha mazungumzo na kuboresha uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Kusini na kuondoa silaha za nyuklia kutoka Rasi wa Korea.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumapili kuwa Marekani itakuwa tayari kukutana na Korea Kaskazini lakini akasisitiza kuwa Korea ni lazima iondoe zana zake za nyuklia.

Hata hivyo Korea Kaskazini ambayo imesema inataka kufanya mazungumzo na Marekani, imesema kuwa ni hatua ya "kishenzi" kuwa Marekani inataka kuwepo masharti.

Haijulikani ni nani atawakilisha Marekani ikiwa mkutano kama huo utafanyika.

Mjumbe mkuu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini Joseph Yun alitangaza uamuzi wake wa kustaafu mapema wiki iliyopita.

Wadadisi wanaamini kuwa Bw Yun alikuwa akipendelea sana suluhu ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.