Aidha, badhi ya walimu wa shule za Msingi na Sekondari katika Kijiji hicho, wamesema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwathiri utendaji wao wa kazi kwani wamekuwa wakienda shule kutimiza majukumu yako kwa hofu.
Wakizungumza na Channel Ten kwa nyakati tofauti wakazi hao ambao wanapakana na eneo tengefu la wanyamapori la WMA wameiomba serikali kuchukua hatu za haraka kuwadhibiti wanyama hao, kwani kwa sasa wanaishi kwa hofu na kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali ikiwamo kilimo.
Aidha, wamesema wanyama hao wamekuwa wakishambulia kwa kasi mazo yako, ikiwamo mahindi, choroko na mazao mengine ya biashara na kuwaacha wakiwa hawajui la kufanya.
Akizungumzia hali hiyo, Mbunge wa Jimbo la Kisesa, LUHAGA MPINA amesema amepokea taarifa za wanachi hao na kwamba atawsiliana kilio cha wanachi hao kwa Waziri wa Mali asili na Utali, PROESA JUMANNE MAGHEMBE ili kuhakikisha wanyama hao wanadhibitiwa.
0 comments:
Post a Comment