Saturday, 5 August 2017

Neymar aanza mambo PSG


Mshambuliaji mpya wa Paris Saint-Germain, Neymar leo ameanza mbwembwe na kutinga katika mazoezi ya klabu hiyo ingawa hataweza kuichezea timu hiyo katika mchezo wa ufunguzi wa Ligue 1 kutokana na usajili wake kutokamilika.

PSG ilimtambulisha mwanasoka huyo ghali duniani kwenye vyombo vya Habari jana baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 200 kutoka Barcelona.

Neymar aliweka wazi mbele ya umati wa watu kwamba alikuwa tayari kucheza Uwanja Parc De Princes dhidi ya Amiens kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Ufaransa.

Pamoja na hayo, taarifa nchini Ufaransa zinasema kwamba bodi ya soka nchini humo (LFP), ilikuwa haijapata risiti ya uhamisho wa kimataifa hadi usiku wa jana ili kumsajili Neymar aweze kucheza leo mchana.

La Liga wamekuwa wakilalamikia sana uhamisho huo siku za karibuni hadi Rais wake, Javier Tebas akasema watafungua mashitaka Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kupinga matumizi mabaya ya fedha yaliyofanyika kumuhamishia Neymar Ligue 1 kutoka Hispania.

0 comments:

Post a Comment