Sunday, 2 July 2017

Wakulima wa zao la Karanga waiomba serikali kuwajengea viwanda vya kukamua mafuta.


Wakulima wa Karanga katika wilaya za Nanyumbu na Masasi Mkoani Mtwara wameiomba serikali kuwajengea viwanda vya kukamua mafuta ya ili kuongeza thamani ya zao hilo ambalo licha ya uzalishaji wake kuongezeka limeendelea kukosa soko kila mwaka na hivyo kusababisha baadhi ya wakulima kuacha kulima karanga.

Wakizungumza na Radio One Stereo  iliyowatembelea baadhi ya wakulima  wa karanga wamesema licha ya serikali kuwatumia watafiti kutoka Taasisi ya Kilimo Naliendele katika kuzalisha mbegu bora za zao hilo na kuonesha kufanya vizuri, bado  masoko ni tatizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dakta. OMAR MPONDA amesema mbegu zilizotafitiwa zimeonesha kufanya vizuri hivyo wakulima wanahitaji kusaidiwa.

Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Nanyumbu Bwana HAMISI DAMUMBAYA  amesema mazao mchanganyiko ikiwemo karanga yamefanikiwa kuiingizia halmashauri ushuru wa zaidi ya Shilingi Milioni Mia-Tatu na kusisistiza halmashauri iko katika harakati za kutafuta masoko.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment