KUKOSEKANA kwa ofisi ya mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)Wilayani Chato Mkoa wa Geita kumesababisha ukusanyaji wa mapato kusuasua hali iliyosababisha mamlaka hiyo kukusanya kiasi cha sh.Milion 568 pekee katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 unaomalizika ifikapo julai mosi mwaka huu.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa ameyasema hayo kwenye hafla ya uzinduzi wa ofisi ya mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)Wilaya ya Chato mkoani hapa na kuagiza Mamlaka hiyo kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato ya serikali yanayotokana na kodi mbalimbali.
Sambamba na hilo,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepongeza hatua ya mkoa wa Geita kukusanya fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 13.2 sawa na asilimia 93,kwenye mwaka wa fedha 2016/2017 wakati malengo ilikuwa ni kukusanya Bilioni 13.9 na kuziagiza ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)kote nchini kutowatoza fedha za majengo wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea.
0 comments:
Post a Comment