Monday 5 March 2018

Sh. Bilioni 287 zapitishwa kwenye Bajeti ya Manispaa ya Ilala


BARAZA la Madiwani Manispaa ya Ilala imepitisha bajeti ya sh.bilioni 287 katika mwaka fedha wa 2018/2019 ikilinganishwa bajeti iliyopita ya 2017,2018 ya sh.bilioni 124.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mchumi wa Manispaa hiyo, Ando Mwanduga amesema kuwa bajeti hiyo katika sehemu kubwa ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Mwanduga amesema kuwa fedha hizo zitapatikana katika makundi mawili ya ruzuku pamoja na vyanzo vya ndani ambapo hakuna mwananchi atakayeonewa katika bajeti hiyo.

Amesema kuwa chanzo cha mapato ya ndani ni wanatarajia kukusanya sh.bilioni 56.8 ambapo na fedha nyingine zitakuwa ni za ruzuku.Mwanduga amesema kuwa kila diwani anataka kuwa na mradi katika kata yake lakini haiwezikani kutokana na uwezo wa manispaa.

Amesema kuwa bajeti hiyo itatekelezeka ni pamoja na kuwa na vyanzo hivyo viwili vya ruzuku na mapato ya ndani na asilimia 60 ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika kutekeleza miradi.

Aidha amesema kuwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya elimu bure kwa manispaa imethubu ikiwa ni pamoja na kujenga shule nne pamoja na kufanya ukarabati kwa bajeti iliyoishia 2018.


0 comments:

Post a Comment