Monday 5 March 2018

Kocha wa Township Rollers afunguka kuhusu kuifahamu Yanga


Jumanne ya March 5 2018 wapinzani wa Yanga katika michuano ya club Bingwa Afrika Towship Rollers ya Botswana walijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kukubali kuongelea mchezo dhidi ya wenyeji wao Yanga utakaochezwa kesho March 6 2018.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Township Rollers, Nikola Kovazovic aliongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mchezo huo na alikuwa radhi kujibu swali je anaifahamu Yanga ambayo anacheza nayo kesho.

“Katika mpira wa kisasa wa kiwango cha juu kama club Bingwa Afrika hutaweza kupata matokeo kama hutokuwa unafahamu walau hata kwa uchache mpinzani wako unayekwenda kucheza nae, hivyo sisi tunamfahamu mpinzani wetu kitu ambacho kitatusaidia kupata matokeo chanya” Nikola Kovazovic

0 comments:

Post a Comment