Thursday, 22 June 2017

JKT yawaaswa vijana kutotumia mafunzo kufanya uhalifu.


Vijana waliomaliza mafunzo ya jeshi la kujenga taifa operesheni Magufuli katika kikosi cha JKT Bulombora Kigoma, wametakiwa kutotumia mafunzo waliyoyapata vibaya kwa kufanya uhalifu na matendo ambayo yako kinyume na uzalendo wa nchi.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya uvinza Mwanamvua Mrindoko baada ya kukagua Gwaride wakati akifunga mafunzo ya JKT kwa vijana karibu elfu moja wa kujitolea ambapo amesema taifa na jamii linawategemea waende kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali ili kuleta maendeleo.

Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa jeshi la kujenga taifa nchini kanali hawa kodi amesema jeshi hilo litaendelea kuboresha mtaala wa mafunzo ili kuhakikisha vijana wanaopitia jkt wanatumia ujuzi wao kuongeza uzalishaji na kutunza amani katika jamii.

0 comments:

Post a Comment