Home »
Michezo
» Shaffih Dauda, Mwenyekiti Drfa wakamatwa na Takukuru
Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo wagombea wa uchaguzi katika nafasi mbalimbali za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamekamatwa jijini Mwanza.
Baadhi ya waliokamatwa ni pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM, Shaffih Dauda, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Almas Kasongo.
Imeelezwa walikamatwa jana saa tatu usiku jijini humo wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ikiwa ni kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma.
Wengine waliokamatwa ni pamoja na Elias Mwanjale, Leonald Malongo, Effam Majinge, Osuri Kasuli, Richard Kayenzi, Lazack Juma na Kelvin Shevi.
Msemaji wa Takukuru jijini hapa, Ernest Makale amethibitisha kukamatwa kwao na kusema wamehojiwa.
“Tumewahoji na kuwaachia kwa dhamana, sasa uchunguzi unaendelea,” alisema.
Imeelezwa watuhumiwa walisema kwamba walifika jijini Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup jijini humo.
Related Posts:
TASWIRA NNE ZA DOGO BRADLEY WAKATI WA UHAI WAKEHabari si njema katika familia ya soka ya England na duniani kote, nayo ni kifo cha mtoto Bradley Lowery.Bradley shabiki namba moja wa Sunderland na rafiki namba moja wa mshambulizi mkongwe wa Sunderland na England, Jermain D… Read More
USAJILI:LECEISTER CITY YAMNASA MWENYE EUROPA LIGI TATULeceister,England.MABINGWA wa zamani wa ligi kuu ya soka nchini England,Leceister City wamekiongezea uimara kikosi chao tayari kwa msimu ujao kwa kumsajili nahodha wa Sevilla ya Hispania,Vicente Iborra kwa ada ya £12m.Iborra … Read More
KANSA YAMTIBULIA KIPA NAMBA MOJA NIGERIANigeria.KIPA namba moja wa timu ya taifa ya Nigeria,Super Eagles, Carl Ikeme anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kisichojulikana ili kupatiwa matibabu ya kina baada ya kugundulika kuwa ana maradhi hatari ya Kansa.Ikeme… Read More
KELECHI IHEANACHO AKARIBIA KUTUA LEICESTER CITYKLABU ya Leicester City ipo karibuni kabisa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Kelechi Iheanacho kutoka Manchester City, zote za England kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25, lakini dili hilo linaweza kuchukua… Read More
HISTORIA UJERUMANI YATWAA UBINGWA WA MABARA
Timu ya taifa ya Ujerumani imetwaa taji la kombe la mabara baada ya kuishinda Chile kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Saint Petersburg nchini Urusi.
Mshambuliaji Lars Stindl ndie aliyeifungia Ujerum… Read More
0 comments:
Post a Comment