Friday, 7 July 2017

USAJILI:LECEISTER CITY YAMNASA MWENYE EUROPA LIGI TATU



Leceister,England.

MABINGWA wa zamani wa ligi kuu ya soka nchini England,Leceister City wamekiongezea uimara kikosi chao tayari kwa msimu ujao kwa kumsajili nahodha wa Sevilla ya Hispania,Vicente Iborra kwa ada ya £12m.

Iborra ,29,raia wa Hispania anayecheza nafasi ya kiungo cha ulinzi amejiunga na Leceister City kwa mkataba wa miaka minne baada ya kufuzu vipimo vyake vya afya.

Leceister City imeamua kumsajili Iborra aliyekuwa nahodha wa Sevilla katika misimu miwili iliyopita,ili kuiongezea uimara safu yake ya kiungo ambayo imekuwa ikipwaya tangu kuondoka kwa Mfaransa,NG'olo Kante aliyejiunga na Chelsea mwezi Julai mwaka jana.

Iborra ameiacha Sevilla akiwa ameisaidia kutwaa ubingwa wa michuano ya Europa League mara tatu huku akifanikiwa kuichezea klabu hiyo jumla ya michezo 169 tangu alipojiunga nayo mwaka 2013 akitokea Levante.

Iborra anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Leceister City katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya baada ya beki wa kati, Harry Maguire aliyetua kwa £17m akitokea klabu iliyoshuka daraja ya Hull City.

0 comments:

Post a Comment