Nigeria.
KIPA namba moja wa timu ya taifa ya Nigeria,Super Eagles, Carl Ikeme anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kisichojulikana ili kupatiwa matibabu ya kina baada ya kugundulika kuwa ana maradhi hatari ya Kansa.
Ikeme,31,ambaye amekuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Super Eagles tangu kustaafu kwa mkongwe Vincent Enyeama Octoba 2015 amegundulika kuwa na tatizo hilo jana Alhamisi kwenye zoezi la uchuguzi wa afya lililokuwa likifanywa na madaktari wa klabu yake ya Wolves kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi daraja la kwanza nchini England.
Hii ina maana kwamba sasa Wolves italazimika kuingia sokoni katika kipindi hiki cha usajili kumsaka mbadala wa Ikeme ambaye msimu uliopita aliichezea klabu hiyo michezo 33.
Ikeme anaingia kwenye orodha ndefu ya wachezaji ambao maisha yao ya soka yamekutana na kigingi kigumu cha maradhi ya kansa.Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana Uganda ilimpoteza kipa wake Abel Dhaira kwa maradhi hayo hayo.
0 comments:
Post a Comment