Saturday, 8 July 2017

Malinzi ajiuzulu Urais TFF Akiwa Rumande



RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amejiuzulu wadhifa wake wa Ujumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Kupitia kwa wakili wake, kampuni ya Rwegoshora, Malinzi amewaandikia barua FIFA kuwataarifu kujitoa kwenye Kamati hiyo kutokana na kuwa mikononi mwa dola kwa sasa.

Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga.
wapo rumande hadi Julai 17, upepelezi wa kesi yao utakapokamilika baada ya kunyimwa dhamana Julai 3 katika kesi inayowakabili.

Watatu hao walipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza Juni 29 na kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam.

Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isawafo Mwanga.

Katika kesi hiyo, Serikali inawakilishwa na jopo la mawakili watano, wakiongozwa na Pius Hila huku upande wa washtakiwa ukiwakilishwa na mawakili watano, wakiongozwa na Jerome Msemwa.

Mawakili hao watano kwa pamoja wameshindwa kuafikiana ili washitakiwa wapatiwe dhamana.
Malinzi aliingia madarakani TFF Oktoba mwaka 2013 baada ya kupata kura 72 kati ya 126 zilizopigwa akimshinda aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Athumani Nyamlani.

Lakini baada ya kesi hii kuanza kuunguurma na kuwekwa rumande, Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kumteua Makamu wake, Wallace Karia kukaimu Urais wa shirikisho hilo.

Lakini kwa mwenendo wa kesi, Malinzi ndiyo kama amekwishaaga TFF, kwani uchaguzi unatarajiwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma naye hatashiriki tena kutokana na kukosekana kwenye usaili.

Related Posts:

  • Sijasaini mkataba Simba - AishiMlinda mlango wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Aishi Salum Manula, amekanusha kusaini na Klabu ya Simba huku akiongeza kuwa vipo vilabu vingi vya hapa nchini alivyofanya navyo mazungumzo na muda ukifika itajulikana na … Read More
  • Wachezaji bongo tusiogope kwenda nje - MaguliMshambuliaji wa kimataifa anayeitumikia klabu ya Dhofar SC ya nchini Oman, Elias Maguli amewataka vijana wa Kitanzania wanaotaka kuendeleza vipaji vyao, nje ya nchi kujaribu pale wanapopata nafasi na sio kukata tamaa.Maguli a… Read More
  • Breaking News: Jamali Malinzi hatoweza kushiriki uchaguzi TFFRais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais.Malinzi hataweza kwa kuwa kesi iliyomfikisha mahakamani leo itasikilizwa tena Jumatatu Julai 3 na Malinzi atakaa rumande hadi siku hiyo.Usaili wa viongozi wanao… Read More
  • Mchezaji wa Lever Pool atembelea watoto yatima ZanzibarFamilia ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England jana Jumamosi imetembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa, Unguja.Sakho amefuatana na mke wake Madna na watoto… Read More
  • Okwi Atema ChecheMshambuliaji wa zamani wa kikosi cha Simba Emmanuel Okwi ambaye jana amerejea rasmi katika kikosi hicho baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Simba amefunguka na kusema amekuja kupambana kuhakikisha kuwa Simba inapata ubingw… Read More

0 comments:

Post a Comment