Monday, 26 June 2017

JOSEPH KABILA Tutaendelea kuzungumzia hali ya kisiasa kufikia muafaka

  
Afrika Kusini imeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC pamoja na wanasiasa wa upinzani kuendeleza mazungumzo yenye lengo la kupata muafaka wa kisiasa katika taifa hilo.

Rais Jacob Zuma ametoa rai hiyo baada ya kukutana na Rais Joseph Kabila na kuelezea matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano ya kisiasa yaliyotiwa saini Desemba mwaka jana kati ya serikali na upinzani.

Kabila amesema serikali yake itaendeleza mazungumzo hayo ili kufanikisha amani nchini humo kwa lengo la kufanikisha uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, ambao hata hivyo haijaelezwa ni lini utafanyika.

Wapinzani wameendelea kulaani uongozi wa Kinshasa, kwa kukataa kutekeleza mkataba wa kisiasa na kufanyika kwa uchaguzi Mkuu kwa madai kuwa Rais Kabila hataki kuondoka madarakani.

Kutotekelezwa kikamilifu kwa mkataba huo, kumechelewesha pia mazishi ya kiongozi maarufu wa upinzani nchini DRC Ettiene Tshisekedi aliyefariki dunia Februari mwaka huu.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment