Monday, 26 June 2017

Waliomuingiza mtu mweusi kwenye jeneza, Mahakamani Afrika Kusini


Hatimaye wakulima wawili weupe wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini, kwa tuhuma za kumsukuma mtu mmoja mweusi na kumuingiza ndani ya jeneza, huku wakitishia kummwagia mafuta ya petroli ili kumteketeza kwa moto akiwa hai.

Washtakiwa hao Willem Oosthuizen na Theo Jackson, walikamatwa Novemba mwaka jana, baada ya video ya kitendo hicho kuzungushwa mitandaoni.

Walisema kuwa, Victor Mlotshwa alipita kwenye shamba lao lililopo katika jimbo la Mpumalanga, bila ya kuwa na idhini, na kwamba hatua waliyochukuwa ilikuwa ni kumuadhibu.

Katika kusikilizwa kwa kesi hiyo awali, Jaji wa mahakama alisema kuwa wakulima hao walikuwa ni wakatili na waliojaa tabia za ubaguzi wa rangi.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment