Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel ametangaza kubatilisha 'haki' ya Wapalestina kutembeleana katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kufuatia mauaji ya mwanajeshi wa kike wa utawala huo wa Kizayuni.
Katika kikao cha baraza la mawaziri leo Jumapili, Benjami Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala khabithi wa Israel amesema Tel Aviv imefutilia mbali haki ya Wapalestina kutembeleana, ambayo ilipasishwa katika kipindi hiki cha funga.
Kadhalika Netanyahu amesema jeshi la Israel linajiandaa kufanya operesheni kali ya kuwasaka na kuwaangamiza waliohusika na mauaji ya mwanajeshi huyo wa kike.
Ijumaa alasiri, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwapiga risasi na kuwaua shahidi vijana wanne wa Kipalestina kwa tuhuma za kumuua askari huyo wa Israel kwa kumchoma visu.
Wanawake wa Kipalestina katika maandamano dhidi ya Israel
Kwa mujibu wa televisheni ya al-Mayadeen, vijana kadhaa Wapalestina waliwavamia kwa visu wanajeshi wa Kizayuni na kukabiliana nao katika Mlango wa Babul Amud wa Msikiti wa al-Aqsa, katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.
Katika makabiliano hayo vijana Wapalestina walimuangamiza mwanajeshi mmoja wa kike wa utawala wa Kizayuni na kuwajeruhi wengine wawili. Kufuatia tukio hilo, utawala wa Kizayuni umeimarisha doria zake za kidhalimu katika njia zote zinazoelekea katika mji huo unaokaliwa kwa mabavu wa Quds Tukufu.
0 comments:
Post a Comment