Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Algeria wamesisitiza juu ya udharura wa kutatuliwa kwa njia za amani hitilafu na mivutano ya kieneo.
Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na mwenyeji wake Abdul-Qader Messahel wamesisitiza hayo katika mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari na kueleza kwamba, kuna haja kwa hitilafu za kieneo ukiwemo mgogoro ulioibuka hivi karibuni miongoni mwa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kupatiwa ufumbuzi wa kieneo na hivyo kutoruhusu uingiliaji kutoka nje.
Dakta Zarif amesema katika mkutano huo na waandishi wa habari kwamba, ufumbuzi wa migogoro ya kieneo haupaswi kutafutwa kutoka nje kwani uingiliaji wa kigeni hupelekea migogoro hiyo kuchukua muda mrefu kutatuliwa na hata wakati mwingi kuivuruga zaidi.
Dakta Zarif alipokuwa akipanda ndege mjini Tehran tayari kwa ajili ya kuelekea Algeria
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa migogoro ya eneo ni kwa manufaa ya makundi ya kigaidi na utawala wa Kizayuni wa Israel na akasisitiza kwamba, Iran haitatumbukia na kunasa katika njama za maadui na katu haitawaandalia uwanja wa kutumia vibaya mambo Wazayuni maghasibu.
Kwa upande wake Abdul-Qader Messahel, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria amebainisha kwamba, kutatuliwa matatizo ya mashariki ya Kati kupitia njia ya mazungumzo ndilo jambo linalopewa kipaumbele na Algiers katika sera zake za kigeni. Dakta Zarif leo amewasili Algeria akiwa katika safari yake ya kuzitembelea nchi kadhaa za Kiafrika ikiwemo Mauritania na Tunisia.
0 comments:
Post a Comment