Thursday, 20 July 2017

Waziri Kairuki: Uhamisho wa watumishi wa Umma ufanyike kwa umakini


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amezitaka Taasisi za Serikali kuratibu suala la uhamisho wa watumishi wa umma kwa makini pale inapohitajika kufanya hivyo Ili kuepuka kero na usumbufu kwa watumishi.

Waziri Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala eneo la Segerea, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema uhamisho lazima ufanyike kwa mtumishi wa umma endapo kukiwa na sababu za msingi sana. “Naomba ieleweke kuwa uhamisho una taratibu zake hivyo kila mwajiri ni mwajiri akazifuata.” Mhe. Kairuki alisisitiza.

Ameongeza kuwa imebainika wapo baadhi ya watumishi wa umma wanawasilisha sababu mbalimbali kwa waajiri kuomba kuhama wakiwa na nia ya kukwepa kukaguliwa sifa zao za elimu.

0 comments:

Post a Comment