Thursday, 20 July 2017

Naibu Waziri Mpina afanya ziara ya kushtukiza usiku kubaini uharibifu wa mazingira


Katika hali isiyoya kawaida, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amefanya ziara ya Oparesheni maalum kwa kushirikiana na jeshi la Police kitengo cha FFU ili kuweza kubaini uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa uchimbani na uchotaji wa mchanga katika vyanzo vya maji na maeneo mengine.

Akiwa katikati ya Mto Mpigi uliopo katika mpaka wa Dar es salaam na Bagamoyo usiku wa kuamkia leo, naibu Waziri Mpina alisema kuwa watu wanaochimba na kuchota mchanga kiholelea watachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria, kutaifishwa kwa magari yao na hata kufikishwa mahakamani.

“kama mnavyoona hapa na kama tulivyosikia kutoka kwa mtu wa DAWASA haya mabomba ya maji yanayopita katika mito yanaharibika kutokana na shughuli hizi na serikali inaweza kuingia gharama kubwa sana kurekebisha mabomba haya kama bomba hili Mtaalam amesema hapa itagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 kutengeneza bomba hili.” Alisema Mpina.

Aidha Mpina alisema ukiachilia mbali uharibifu wa Miundo Mbinu hiyo ya Maji pamoja na Mazingira wananchi wnaweza pia kukosa maji kwa takribani muda wa wiki mbili

0 comments:

Post a Comment