Thursday, 27 July 2017

Umesikia Habari ya Simba Kuchapwa Bao 7 Mechi ya Kirafiki?



Uongozi wa Klabu ya Simba wenye makao makuu yake Msimbazi Jijini Dar es Salaam umekanusha vikali taarifa iliyotembea katika mitandao ya kijamii inayodai timu hiyo imechapwa bao 7-0 katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Royal Eagles ya nchini Afrika Kusini walipoweka kambi yao.

Hayo yameweka bayana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa timu hiyo Haji Manara na kusema kama kweli wamechezea kichapo hicho kutoka kwa timu ya daraja la kwanza hakuna mtanzania asingeweza kuona matokeo hayo katika vyombo vya habari kutokana na sasa utandawazi umetawala.

"Kiukweli Simba haina rekodi za hovyo kama hizo kokote inapocheza duniani na haijawahi kufungwa na klabu yoyote idadi ya magoli kama hayo, kama zilivyo timu nyingine nchini hususan Klabu ambayo mashabiki wake ndiyo wanaozusha upuuzi huo", amesema Manara.

Kwa upande mwingine, Manara amewataka watanzania na mashabiki wa wekundu wa msimbazi watambue kuwa siku zote walizokuwa huko nchini Afrika Kusini, benchi lake la ufundi limejikita katika kutengeneza miili ya wachezaji kistamina ili iweze kufanya vizuri katika michezo yake ambayo ipo usoni kuanza.

Related Posts:

  • Breaking News: Jamali Malinzi hatoweza kushiriki uchaguzi TFFRais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais.Malinzi hataweza kwa kuwa kesi iliyomfikisha mahakamani leo itasikilizwa tena Jumatatu Julai 3 na Malinzi atakaa rumande hadi siku hiyo.Usaili wa viongozi wanao… Read More
  • Taifa Stars kukipiga na Mauritius leoTimu ya mpira wa miguu Tanzania, Taifa Stars inalizimika kupapambana kadri ya uwezo wao leo ili kushinda na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Angola mchezo uliyochez… Read More
  • Manny Pacquiao kuzipiga jumapiliManny Pacquiao (kushoto) akinyoosha mkono wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea pambano lake kutetea mkanda wake wa WBO uzito wa Welter dhidi ya Jeff Horn (kulia) mjini Brisbane, Jumapili… Read More
  • Sijasaini mkataba Simba - AishiMlinda mlango wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Aishi Salum Manula, amekanusha kusaini na Klabu ya Simba huku akiongeza kuwa vipo vilabu vingi vya hapa nchini alivyofanya navyo mazungumzo na muda ukifika itajulikana na … Read More
  • Cristiano Ronaldo afurahia kupata pachaSaa kadhaa baada ya kuiongoza Ureno katika mechi ya nusu fainali ya kombe la mashirikisho ambapo ilishindwa nchini Urusi, Cristiano Ronaldo ametangaza kupata pacha.Siku nne zilizopita vyombo vya habari nchini Ureno vilitangaz… Read More

0 comments:

Post a Comment