Saturday, 1 July 2017

Naibu Waziri atoa siku 15 Kiwanda cha mikeka Vingunguti kurekebisha mfumo wa utoaji moshi.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira Luhaga mpina ametoa siku 15 kwa uongozi wa kiwanda cha Oky Past kilichoko Vingunguti kufanya marekebisho kwenye mfumo wa utoaji moshi katika kiwanda hicho kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wakazi wa vingunguti.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ambacho kinatengeneza badhaa aina ya mikeka kwa kutumia betry zilizotumia amesema serikali hii inatoa kipumbele kwenye uendelezwaji wa viwanda hasa  vinavyouza bidha  nje ya nchi lakini pia wanasisitiza viwanda hivyo vifuate sheria ili uwekezaji huo usilete madhara.

Amesema viwanda vinatakiwa kutoa taarifa ya  ubora wa hewa kila baada ya miezi  mitatu kwa baraza la mazingira NEMC hivyo ametoa muda wa siku 15 na kuwashauri wenye kiwanda hicho kuangilia uwezekano wa kufanya mazungumzo na wenye nyumba ziliojirani kabisa na kiwanda hicho pamoja na serikali ili kuangalia uwezeko wa kununua  nyumba hizo.

Nae Ofisa Mhakiki wa kiwanda hicho Bw Ankleti Pereira amesema hilo ni eneo la viwanda na kwamba swala la moshi haliepukiki kwenye viwanda.

0 comments:

Post a Comment