Kohl aliwahi kuwa kansela wa Ujerumani na alifariki dunia Juni 16 akiwa na umri wa miaka 87.
Kutoka Strasbourg, mwili wake utasafirishwa kurudi nyumbani Ujerumani na atazikwa katika makaburi ya Kanisa Kuu la Kikatoliki katika mji mkongwe wa Speyer. Kiongozi huyo hatakumbukwa tu kwa mafanikio yake kisiasa, lakini pia kwa heshima kubwa aliyopewa wakati wa mazishi.
Kohl anakuwa kiongozi wa kwanza kuandaliwa mazishi rasmi ya Umoja wa Ulaya kutokana na mchango alioutoa katika kuliunganisha bara hilo baada ya vita kuu ya pili ya dunia.
Mbali ya viongozi waliokusanyika Strasbourg, wengine walibaki Ujerumani. Mazishi ya Kohl yalikumbwa na utata baada ya mjane wake kukataa asifanyiwe mazishi ya kitaifa.
0 comments:
Post a Comment