Home »
Michezo
» Hatimaye Maradona akiri bao lake la ''hand of God'' halikufaa kukubalika
Diego Maradona ameunga mkono utumiaji wa kanda za video licha ya kukiri kwamba bao lake la ''Hand of God'' dhidi ya Uingereza 1986 halikufaa kukubalika.
Maradona alitumia mkono wake kufunga bao ambalo liliisaidia Argentina kuishinda Uingereza 2-1 katika robo fainali ya kombe la dunia miaka 31 iliopita.
''Kwa kweli mimi hukumbuka bao hilo kila mara ninapounga mkono utumizi wa teknolojia'' ,Maradona aliambia Fifa.com.
''Nilifikiria kuhusu bao hilo na kwa kweli bao hilo halikufaa kuidhinihswa''.
Maradona anasema kuwa alifaidika kutokana na ukosefu wa teknolojia katika kombe la dunia na haikuwa mara moja bali mara mbili.
''Nitakwambia kitu chengine -katika kombe la dunia la 1990 nilitumia mkono wangu kuondoa mpira uliokuwa karibu kuingia katika goli letu dhidi ya taifa la Usovieti.
''Tulikuwa na bahati kwa sababu refa hakuona.Hakukuwepo na teknolojia wakati huo lakini sasa ni mambo mengine''.
Related Posts:
Hatimaye SportPesa yaikabidhi Yanga jezi zaoHatimaye Yanga wamekabidhiwa jezi zao za msimu ujao na wadhamini wao SportPesa.Yanga ilicharuka baada ya jezi zao kukabidhiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom ambao ni wadhamini wa Ligi Kuu Bara.Lakini leo, Yanga wam… Read More
Mo Farah afanya maajabu katika mbio ndefuSasa hakuna ubishi tena kwamba Mo Farah wa Uingereza ndiye Mfalme wa mbio ndefu za Mita 10000.Farah mwenye asili ya Somalia ameibuka na ushindi katika mashindano ya Ubingwa wa dunia yaliyofanyika jijini London, usiku wa kuamk… Read More
Yanga yaishindilia Singida United 3-2YANGA SC imetoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Singida United katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Shujaa wa Yanga katika mchezo wa leo alikuwa ni kiungo mshambuliaji, Emmanuel Mar… Read More
Sol Campbel tayari ametua nchini kwa ajili ya ziara Beki kisiki wa zamani wa Arsenal, Sol Campbel tayari ametua nchini kwa ajili ya ziara ambayo ni mwaliko wa SportPesa Tanzania.Campbell ametua na kupokelewa na wenyeji wake SportPesa na baadaye mashabiki wa Arsenal ambao… Read More
Neymar aanza mambo PSGMshambuliaji mpya wa Paris Saint-Germain, Neymar leo ameanza mbwembwe na kutinga katika mazoezi ya klabu hiyo ingawa hataweza kuichezea timu hiyo katika mchezo wa ufunguzi wa Ligue 1 kutokana na usajili wake kutokamilika.PSG … Read More
0 comments:
Post a Comment