Home »
Michezo
» Baada ya CAF kuivua Zanzibar uanachama, bendera yake yayeyuka visiwani humo

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza kuifutia Zanzibar unachama iliyoutoa kwake, lakini siku chache baadaye, bendera ya shirikisho hilo, haijulikani ilipo visiwani humo.
Bendera iliyokuwa mbele ya ofisi za Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), imetolewa na inaelezwa imeshushwa lakini kila ofisa, anasema hajui ilipo!
Tangu ilipotangazwa Zanzibar imepata uanachama wa Caf Machi 16, mwaka huu, bendera ya Caf ilikuwa ikipepea katika Uwanja wa Amaan sehemu ya VIP nje kwenye bustani ndogo, hiyo ilikuwa ni kuashiria ya kuwa Zanzibar ni mwanachama wa kudumu namba 55 wa Caf.
Uamuzi wa kufutiwa uanachama ulitolewa Ijumaa iliyopita nchini Morocco wakati Kamati ya Utendaji ya Caf ilipokutana huku Rais wa ZFA, Ravia Idarous Faina, Katibu Mkuu wa ZFA, Mohd Ali Hilali ‘Tedy’ na Kocha wa Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman ‘Morocco’ nao wakiwepo.
Tamko hilo la kuondolewa uanachama limekuja wakati Hatua ya Nane Bora ya Ligi Kuu ya Zanzibar ikiendelea ambapo baadhi ya mashabiki wameanza kukata tamaa ya kufika uwanjani kutokana na majonzi yanayoendelea.
Related Posts:
La Liga waendelea kukomalia pesa za PSG, waipa UEFA msimu mmoja kuwatimua laa sivyo watakwenda mbali zaidi
Shirikisho la soka nchini Hispania La Liga liliwahi kulikataa dau ambalo PSG walilitoa wakati wa usajili wa mshambuliaji wa Barcelona Neymar wakisisitiza kwamba kiasi hicho cha pesa ni kikubwa kuliko uwekezaji wa PSG.
… Read More
Kuelekea Dar derby, takwimu zinaonesha Lwandamina ni kibonde kwa Omogsemiosonyo5.blogspot.comMechi ya Yanga vs Simba itakayochezwa October 28, 2017 inazalisha mechi nyingine ndani yake (yani mechi ndogo ndani ya mechi kubwa).Leo tuanze na mechi ya makocha (George Lwandamina wa Yanga vs Joseph … Read More
EVERTON KAMA ULIVYOSIKIA; KOCHA MPYA, MAISHA YALEYAKE, YACHAPWA 2-0 NA LEICESTER CITYLeicester: Schmeichel, Simpson, Morgan, Maguire, Fuchs, Mahrez (Okazaki 75), Ndidi, Iborra, Chilwell (Albrighton 83), Gray, Vardy (Iheanacho 89)Subs not used: King, Hamer, Dragovic, SlimaniGoalscorers: Vardy 18, Kenny og 29Ev… Read More
Cristiano Ronaldo anataka kushinda tuzo 7 za dunia na haya ndio matarajio yake katika World Cup 2018semiosonyo5.blogspot.comCristiano Ronaldo alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa FiFA kwa mara ya pili mfululizo jana jijini London, na nahodha wa Ureno jana baada ya kumalizika kwa shughuli ya ugawaji wa tuzo alifanya mahoj… Read More
Ni Wakenya Rock City Marathon 2017Abrahamu Too kutoka Kenya ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza leo baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini… Read More
0 comments:
Post a Comment