Wednesday, 12 July 2017

Azam kucheza mechi tatu Nyanda za Juu Kusini

Category: 
Team: 
Azam FC
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inaendelea kujiweka sawa kuelekea msimu ujao, habari njema ni kuwa imealikwa kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Iringa na Njombe) kucheza mechi tatu za kirafiki.
Azam FC inakwenda huko baada ya kupewa mwaliko maalumu na timu ya Mbeya City ya jijini Mbeya, ambayo itacheza nayo mchezo maalumu wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Sokoine Julai 22 mwaka huu.
Mara baada ya mchezo huo, Azam FC itaelekea mkoani Njombe kukipiga na timu iliyopanda msimu huu, Njombe Mji katika mtanange utakaofanyika Uwanja wa Amani Makambako mjini humo Julai 24.
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu uliopita, watamaliza ziara hiyo kwa kuelekea mkoani Iringa kukipiga na timu nyingine iliyopanda daraja, Lipuli mchezo utakaopigwa ndani ya Uwanja wa Samora Julai 26.
Kwa mujibu wa Meneja wa timu, Phillip Alando, kikosi cha Azam FC kitarejea jijini Dar es Salaam Julai 26 mwaka huu na kupata mapumziko ya siku mbili kabla ya kurejea mazoezini Julai 30 mwaka huu.
Mara baada ya kufanya mazoezi kwa siku kadhaa, kikosi hicho kitacheza mechi mbili za kirafiki zitakazopangiwa tarehe baadaye ambazo ni dhidi ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting, zote zikifanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.  

Related Posts:

  • Malinzi ajiuzulu Urais TFF Akiwa RumandeRAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amejiuzulu wadhifa wake wa Ujumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).Kupitia kwa wakili wake, kampuni ya Rwegoshora, Malinzi amewaandikia … Read More
  • Wana Msimbazi mumemsikia Tambwe?SIKU chache baada ya Yanga kumtambulisha Ibrahimu Ajibu aliyetokea Simba, straika wa timu hiyo, Amissi Tambwe amesema kwa usajili walioufanya hadi sasa, anamuonea huruma huruma Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zachar… Read More
  • Mzee Akilimali Yanga amesema 'Wamekwisha"Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Ajibu amejitapa kuwa ujio wa mshambuliaji, Ibrahim Ajibu kutoka Simba kutazidi kuiongezea makali safu yao ya ushambuliaji.Yanga wamekata mzizi wa fitina baada ya Jumatano wiki hii k… Read More
  • Mwakyembe akoleza moto TFFWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kupigilia msumari jambo ambalo linaendelea (TFF) na kusema ni muendelezo ya kampeni ya serikali ya awamu ya tano kusafisha kila sehemu n… Read More
  • PSG YAANZA USAJILI NA BEKIParis,Ufaransa.MATAJIRI wa Ufaransa,Paris Saint-Germain tayari wameanza kumwaga pesa kwenye dirisha hili la usajili barani Ulaya baada ya jioni ya leo kumsajili beki wa kushoto wa Real Sociedad ya Hispania,Yuri Berchiche.Pari… Read More

0 comments:

Post a Comment