Tuesday, 13 June 2017

Spika Job Ndugai Atoa ONYO Kwa Halima Mdee na Ester Bulaya......Atishia Kuwapa Adhabu Kali Zaidi

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo bungeni amewapa onyo wabunge Halima Mdee pamoja na Easter Bulaya akisema kuwa wanapaswa kutambua kuwa Bunge bado linauwezo wa kuwaita na kuwahoji na kuwapa adhabu kali zaidi ya hiyo walionayo sasa.

Job Ndugai amesema kuwa ameamua kutoa onyo hilo kufuatia wabunge hao kufanya malumbano na bunge huku wengine wakitumia maneno ambayo si mazuri hivyo amewashauri kuwa wamewavumilia kwa mengi lakini kama bado huko waliko wanaendelea na tabia hizo wanaweza kuwaita na kuwapa adhabu kali zaidi ya hiyo waliyonayo sasa.

"Wako wenzetu ambao bunge hili liliwachukulia hatua za kinidhamu mbalimbali baadhi yao wamekuwa wakijaribu kufanya malumbano na bunge na baadhi ya kauli zao zimekuwa ni kauli ambazo si nzuri kihivyo, ningependa kuendelea kuwashauri kwamba tumewavulimilia kwa mambo mengi lakini kama bado huko waliko wanafikiri wanaweza kuendelea na tabia hizo huko waliko wajue kabisa bado tunaweza kuwaita, tukawajadili kwenye bunge hili na kuwachukulia hatua kali zaidi ya hii waliyonayo, kama mtu anataka kwenda mahakamani unaalika watu kama mkutano wa hadhara si unaenda tu" alisisitiza Job Ndugaina kuongeza;

"Mimi nawapa onyo tu la jumla kama ni viongozi ni vizuri kuongea lakini ongea vitu ambavyo unataka kuongea lakini ukitaka kupambana na watu wengine nao watataka kupambana na wewe, kwa hiyo mtapimana" alisema Job Ndugai

Spika wa Bunge, Job Ndugai ametoa kauli hii siku moja baada ya kusifiwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa anakwenda vizuri kuwadhibiti watu ambao wanaropoka bungeni na kumwambia kuwa aendelee na moto huo huo ili watu hao wakiropoka nje ya bunge adili nao. 

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliwaadhibu wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya kutohudhuria vikao vyote vya Bunge linaloendelea hadi Bunge la Bajeti 2018/2019 baada ya kuwakuta na hatia ya kudharau mamlaka ya Spika wa Bunge.

Related Posts:

  • Madhara Ya Kuangalia Video Za Ngono (Porn) Na Namna Ya KuachaKuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu, kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto baada ya kuangalia video za ngono.Bahati mbaya tabia ya kuangalia video hizi watu wengi huip… Read More
  • Sugu awashangaa wanachama wa CCMMbunge wa Mbeya Mjini (Chadema),  Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amewashangaa wananchama wa CCM waliolipigia hesabu jimbo hilo, akidai kuwa wanajisumbua kwa sababu walishapoteana tangu mwaka 2010.Akizungumza leo Desemba 20 katik… Read More
  • Makosa dhidi ya binadamu yaongezeka kwa asilimia 0.9Jeshi la Polisi limesema makosa dhidi ya binadamu yanayojumuisha mauaji, kubaka, kulawiti, kunajisi, wizi na kutupa watoto na usafirishaji binadamu yameongezeka nchini.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert … Read More
  • Tambua Madhara ya Ulaji wa ChipsiChips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree.Chips ni chakul… Read More
  • Madhara ya kuvuta SigaraUfutaji sigara huathiri mwili kwa njia tofauti na madhara yake ni makubwa kiafya. Inakadiriwa kuwa, hadi sasa kumegunduliwa kemikali zipatazo 7,000 katika moshi wa sigara ambapo 250 kati ya hizo ni sumu na 70 zinasababisha ka… Read More

0 comments:

Post a Comment