Thursday, 22 June 2017

Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza kiwanda cha viuatilifu vya malaria Kibaha


Rais John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha kutengeneza dawa za kuulia vimelea vya mbu wanaosababisha malaria kilichopo Kibaha, Pwani.

Magufuli amevamia katika kiwanda hicho leo (Alhamisi) katika siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Pwani na kuzipa siku 10 halmashauri, manispaa na majiji nchini kwenda kuchukua dawa hizo za kuua vijidudu vya malaria na kuzipulizia katika maeneo yao yalipo makazi ya watu.

“Sasa mimi nimeshatoa agizo dawa zilipiwe, sasa nione mkurugenzi ambaye atashindwa kutekeleza agizo langu la kufata dawa hizo kwa kipindi nilichotoa, nimesema natoa muda mpaka  mwisho wa mwezi, "amesema Rais Magufuli.

Kadhalika, Rais ameiagiza Wizara ya Fedha kutoa Sh1.3 bilioni  kwa ajili ya kulipia lita 100 ya dawa  hizo za kuua vimelea vya mbu zilizopo katika kiwanda hicho.

Awali, Kaimu Meneja wa kiwanda hicho, Samweli Mziray alimweleza Rais kuwa dawa takribani lita 100 zipo tu kiwandani hapo baada ya wanunuzi wakuuu ambao ni Halmashauri za Wilaya kushindwa kuzinunua kwa madai ya kukosa fedha.

Kadhalika, Mziray amefafanua zaidi na kumweleza Rais kuwa kushindikana kununuliwa dawa hizo kwa wakati kunaweza kusababisha zikaharibika  kwa sababu  zinatakiwa zisihifadhiwe zaidi ya miezi miwili tangu  zinapotengenezwa.

Related Posts:

  • ABIRIA Waomba Kuruhusiwa Kusafiri UsikuAbiria wa mabasi yanayotoka mikoa ya bara yanayopita mkoani Morogoro kuelekea jijini Dar es Salaam wameiomba serikali iruhusu mabasi ya abiria kusafiri baada ya saa sita usiku hasa katika maeneo ambayo sio hatarishi kwa usafi… Read More
  • WABUNGE Tisa Walivyolichangamsha Bunge kwa Hoja, MisimamoDODOMA.Mkutano wa saba uliomalizika mjini hapa wiki iliyopita, haukuacha rekodi ya kufanya mabadiliko makubwa katika Bajeti Kuu ya Serikali pekee, bali pia baadhi ya wabunge kuacha gumzo kutokana na hoja na mambo yao.Mkutano … Read More
  • Hatimaye Prof Jay afunga ndoa leoSiku chache tangu Mbunge wa Mikumi Joseph Haule Aseme kwamba Ndoa yake yakaribia ambapo leo yametimiaMbunge huyo ambaye ni Mkali wa Muziki wa Bongo Hip Hop Prof Jay  amefungua ndoa leo kwenye kanisa la St Joseph Jijini d… Read More
  • Jinsi Ya Kufanya Mambo Magumu Kuwa RahisiNi rahisi kufanikisha jambo lolote, ikiwa jambo hilo utataanza kulifanya mara moja na kuacha kusubiri.Ni rahisi kujifunza kitu kipya kwenye maisha yako, ikiwa utaamua kweli kujifunza kila siku.Ni rahisi kutoka kwenye kushindw… Read More
  • KIMENUKA...Wafuasi 51 wa Chadema Wakamatwa na Polisi, ChatoWafuasi na Viongozi  51 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokamatwa jana Ijumaa  wakiwa kwenye kikao cha ndani wilayani Chato wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.Miongoni mwa waliotiwa mb… Read More

0 comments:

Post a Comment