Thursday, 29 June 2017

CCM Sumbawanga wampongeza Rais Magufuli


RAIS Dr John Pombe Magufuli amepongezwa kwa uzalendo mkubwa alionao kwa nchi na rasilimali zilizoko katika nchi ya Tanzania kiasi cha kuamua kujitoa maisha yake kuitetea nchi ya Tanzania na watu wake kama alivyofanya muasisi wa Taifa hili Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Pongezi hizo na uungwaji mkoano kwa Rais Dr. Magufuli zimetolewa leo ikiwa ni maazimio 17 ya kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Sumbawanga mjini iliyoketi katika mji mdogo wa Mpui wilaya ya Sumbawanga.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wamewaomba Watanzania kumuombea Rais kila mmoja kwa imani yake na kumuunga mkono kwa vitendo.

0 comments:

Post a Comment