Friday, 24 March 2017

Ufafanuzi wa Nape Nnauye kuhusu taarifa zinazomuhusisha yeye na Kinana


Moja kati ya taarifa zilizosambaa leo katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Abdularahman Kinana kuwa ataongea na vyombo vya habari saa nne asubuhi ofisi ndogo ya chama cha CCM Lumumba Dar es Salaam.
Taarifa hizo hazikuwa za kweli lakini uvumi ukaendelea kuenezwa kuwa Kinanaamekatazwa kuongea na waandishi, taarifa ambazo sio za kweli pia huku ikionekana account fake ya Mbunge wa Mtama ambaye ameondolewa katika uwaziri Nape Nnauyendio kaandika katika twitter account yake.

Hii akifafanua kuhusu ujumbe uliyoenezwa kuwa kamuandikia Kinana
Nape Nnauye ametumia ukurasa wake rasmi wa twitter kueleza kusikitishwa kwake na watu wanaozusha taarifa hizo zenye lengo la kumchafua kuhusu katibu Mkuu wa CCMKinanaNape ameandika kuwa hajaandika taarifa hizo zinazomuhusu Kinana.

Kutoka katika twitter ya Nape kuwa ujumbe huu sio wa kwake
FULLVIDEO: Alichokizungumza Nape Nnauye alipokutana na Waandishi wa Habari

0 comments:

Post a Comment