Monday, 20 February 2017

DC Hapi atangaza Kiama kwa wavuvi Haramu


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ametangaza rasmi vita dhidi ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Pwani wa Wilaya ya Kinondoni, ambapo amechoma moto nyavu haramu 77 zenye thamani zaidi ya milioni 60 zilizokamatwa kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi Februari, 2017.
Hapi ametangaza vita hiyo leo katika muendelezo wa ziara yake ya awamu ya pili inayohusisha kata kumi za wilaya hiyo ambapo alikuwa katika Kata ya Mbweni.
DC Hapi pia amemkabibidhi Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, RPC Suzan Kaganda majina ya wavuvi haramu pamoja na viongozi wawili wa serikali wanaotuhumiwa kushiriki katika biashara ya uvuvi haramu.
“Natangaza vita dhidi ya uvuvi haramu katika mialo yote iliyoko katika manispaa yetu, kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama tutatokomeza vita hii,”
“Yeyote mwenye dhana za uvuvi haramu ikiwemo milipuko, mikuki na nyavu haramu aisalimishe bila ya kufanya hivyo popote alipo hayuko salama. Yapo majina ya viongozi wawili aanaoshirikiana na maharamia kutekeleza uvuvi haramu, vita hii itaendelea na majina tutayapeleka katika vyombo vya ulinzi na usalama,” amesema.
Aidha, ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kukamata watakao kutwa na dhana za uvuvi haramu pamoja na wasio kuwa na vibali vya uvuvi.
“Mtu yeyote atakayekutwa na nilipuko au baruti bila vibali akamatwe sababu ipo siku ataitumia kufanyia uhalifu kwa watu badala ya uvuvi,” amesema.                       
DC Hapi amkabidhi majina ya wavuvi haramu RPC Kinondoni, wapo vigogo, achoma nyavu zenye thamani zaidi ya Mil. 60

0 comments:

Post a Comment