Watumiaji wa huduma za nishati na maji katika manispaa ya mtwara mikindani wamelalamikia baadhi ya huduma zinazotolewa na wamiliki wa vituo vya kujazia mafuta wanaodaiwa kuchanganya mafuta na maji pamoja na mamlaka ya maji safi na maji taka mjini mtwara MTUWASA kwa kusambaza maji machafu kwa wateja wake huku maeneo mengi yakikosa huduma ya maji safi na salama.
Wakizungumza katik Mafunzo ya wajibu na haki kwa watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa wakazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, baadhi ya madereva pikipiki za abiria maarufu Bodaboda pamoja na wananchi kwa ujumla wamesema tatizo la kugundua maji katika mafuta ya pikipiki limetokea zaidi ya mara moja huku wengine wakihoji juu ya maji machafu yanayotoka katika mabomba.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha mitambo na usambazaji wa maji(MTUWASA) Lukelo Wandelage alikiri uwepo wa wateja wanaopata maji machafu majumbani huku Mhandisi Goodluck mmari, katibu mtendaji wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za maji na nishati(ewura)Akieleza umuhimu wa elimu itakayosaidia akina mama kuhusiana na huduma za maji.
Mamlaka ya usimamizi wa huduma za nishati na maji ewura kupitia baraza la huduma za watumiaji wa nishati na maji ewura ccc wameendesha mafunzo ya wajibu na haki kwa watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa manispaa ya mtwara.
0 comments:
Post a Comment