Thursday 15 June 2017

“FULL STORY” Matapeli wa vyeti na nyaraka feki, Wakutwa na Mihuri 50 na nyaraka za taasisi za serikali


Idara ya Uhamiaji Tanzania inawashikiliwa watu watano kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka za Serikali na mihuri feki hamsini ambavyo wamekuwa wakivitumiwa kwa utapeli na kuwatengenezea watu barua na vyeti mbalimbali.

Watuhumiwa hao ambaye mwenye umri mdogo ana miaka 55 walikamatwa maeeno ya Posta jijini Dar es salaam baada ya makashero wa Uhamiaji kupata taarifa na kufanya upekuzi kwenye ofisi wanayoitumia na kukutana na nyaraka hizo za kitapeli

Akizungumzia kuhusiana na madhara ambayo yamepatikana kutokana na watu wanaotumia nyaraka za utapeli na vyeti feki, Kamishna wa Uhamiaji anafafanua zaidi.

Hata hivyo watuhumiwa hao ambao wengi wao ni wastaafu wamekana kuhusika na nyaraka na mihuri feki waliyokutwa nayo licha ya kwamba imekutwa kwenye ofisi ambayo wamekuwa wakiitumia .

Watuhumiwa hao wanatarajia kupandishwa mahakamani kujibu mashataka yanayowakabili huku ukaguzi ukiendelea kubaini waliotumia nyaraka na vyeti vya kughushi nao wafikishwe kwenye mkondo wa sheria .

0 comments:

Post a Comment