Thursday 15 June 2017

Moto wateketeza Maduka Matatu na Vitu vyenye Thamani ya Sh.Milioni 300 Bunda Mara


Moto mkubwa umezuka katika Mji wa Bunda mkoani Mara na kuteketeza maduka matatu na stoo za kuhifadhibia bidhaa mali za wafanyabiashara na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Chaneli teni kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumanne Aprili 14 mwaka huu, katika eneo la Nguvu Moja karibu na soko Kuu la mjini Bunda.

Wakizungumza na Chaneli teni mashuhuda wa tukilo hilo wamesema moto huo umeanzia kwenye chumba kimoja na badae kusambaa katika maduka yote yaliyokuwa kwenye jengo moja kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bunda Mjini JOASHI KUNUGA, amesema chanzo cha kuteketea kwa jengo hilo kunatokana na ukosefu wa gari la zima moto.

Aidha, Meneja wa Tanesco katika wilaya ya Bunda, JULIUS FALU amesema haukutokana na hitilafu ya umeme, labda kuna chanzo kingine ambacho bado hakijafahamika.

Katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya wananchi wakageuza tukio hilo kama njia ya kujinufaisha, baada ya kuanza kunywa pombe na vinywaji mbalimbali.


0 comments:

Post a Comment