Siku chache baada ya Rais kupokea ripoti ya Pili ya Uchunguzi ya Usafirishaji Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi, Chama cha mapinduzi CCM mkoa dsm kimeunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na kamati ikiwemo wale wote waliohusika kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa uchunguzi dhidi yao utakaofanyika na vyombo husika.
Akizungumza katika mkutano maalum wa wana CCM wilaya ya Ubungo kuunga mkono hatua za rais Magufuli katika kulinda rasilimali za Nchi kwa manufaa ya wananchi wote, Katibu wa CCM Mkoa wa DSM Alhaj Saad Silawe ametaka hatua kali dhidi ya waliohusika zichukuliwe huku baadhi ya viongozi wa chama hicho wilaya ya Ubungo wakielezea matarajio kuwa watakaobainika wafilisiwe ili fedha zilizopotea zirudishwe na kutumika katika kuboresha huduma za kijamii.
0 comments:
Post a Comment