Thursday 15 June 2017

Kampeni ya nipo tayari, Unicef yaunga mkono kupiga vita udumavu

4bmue6921ceec3n9ok_800C450

Suala la Utapiamlo na udumavu kwa watoto wadogo hasa sehemu za vijini linaonekana kuwa kubwa kutokana na baadhi ya wazazi na walezi kushindwa kuelewa namna ya kuweza kuwaepusha na tatizo hilo watoto hao.

Kutokana na hali hiyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF, kwa kushirikana na wadau ambalimbali wakiwemo wa masuala ya usafi wa mazingira wamekutana na kujadili namna ya kuweza kupunguza au kumaliza tatizo hilo ambalo linakwenda sambamba na usafi wa mazingira.

Tuzie Edwin ni Afisa Lishe wa UNICEF ameeleza kuwa katika kutekeleza kampeni ya NIPO TAYARI ambayo inahamasisha usafi wa mazingira, kwa sasa wana mradi mkubwa ambao unalenga kumaliza tatizo hilo kama anavyoeleza.

Na hapa anaeleza sababu za kujikita katika kupunguza udumavu na usafi wa mazingira.

Kwa upande wa mtaalamu wa lishe kutoka UNICEF MAURO BRERO, ameeleza kuwa bila kuwa na lishe bora pamoja na usafi wa mazingira ni ngumu kufanikiwa, huku mdau wa masuala ya lishe Dokta Generosa Mulokozi, akizungumzia athari zinazoweza kutokea iwapo utaratibu utakiukwa.

0 comments:

Post a Comment