Mabenki pamoja na taasisi za kifedha nyingine zimepewa changamoto ya kupanua wigo wa soko la wateja wanaotumia huduma za kibenki ili ziwafikie wananchi wengi kwani ianadaiwa kuwa ni asilimia 14 tu ya wananchi wote ndiyo wanaotumia huduma hizo licha Tanzania kuwa na idadi kubwa ya mabenki na taasisi za kifedha.
Msajili wa Hazina nchini Dk Osward Mashindano anasema haya akiwa jijini Mbeya wakati akifungua tawi la Benki ya Posta TPB Bank eneo la Mwanjelwa, akisema ni dhahiri kuwa watanzani wengi bado hawajafikiwa na huduma za kibenki.
Lakini pia akasema serikali haitasita kuchukua hatua stahiki kwa viongozi wanaonekana kutaka kuikwamisha tasisisi ya kifedha .
Sabasaba Moshingi ndiye Mtendaji Mkuu wa TPB anawataka wakazi wa mkoa wa Mbeya kutumia fursa za kibenki kwa kukopa fedha hususani kwenye benki hiyo ambayo inakuwa kwa kasi .
(Benki ya Postal TPB imeendelea kufanya vizuri kwa kujenga mtaji kutoka mtaji wa shilingi bilioni 8 mwaka 2010 hadi shilingi bilioni 52 kwa mwaka jana, lakini pia ikiwa imejipanga kuwahudumia watanzia ili kuongeza uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla).
0 comments:
Post a Comment