Wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wamefanya maandamano ya amani katika mji mkuu wa nchi hiyo wakitaka kuachiwa huu kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Waandamanaji hao waliozunguka mitaa ya mji wa Abuja wametoa wito wa kuachiwa huru Sheikh Zakzaky ambaye anahitajia uangalizi wa dharura wa madaktari.
Waandamanji hao pia wameitaka serikali ya Nigeria kutii amri ya mahakama ya nchi hiyo iliyoamuru kuachiwa huru kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo. Wamesema kuendelea kushikiliwa korokoroni Sheikh Zakzaky ni njama iliyopikwa na Saudi Arabia kwa shabaha ya kuangamiza Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria.
Zakzaky baada ya kukamatwa na jeshi la Nigeria
Serikali ya Nigeria inadai kuwa, inaendelea kumshikilia Sheikh Ibrahim Zakzaky kwa shabaha ya kulinda usalama wake, suala ambalo linapingwa na wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.
Mwaka 2015 jeshi la Nigeria lilivamia kituo cha kidini cha Baqiyatullah katika mji wa Zaria huko kwenye jimbo la Kaduna na kumtia nguvuni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky, mke wake na mamia ya wafuasi wake. Mamia ya Waislamu pia waliuawa katika shambulizi hilo.
0 comments:
Post a Comment