Thursday 15 June 2017

UN yalaani mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Somalia


Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amelaani mashambulizi yaliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo.



Michael Keating amelaani mashambulizi yaliyotekelezwa huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia na kutangaza kuwa, hakuna kitendo chochote kinachoweza kuhalalisha kushambuliwa raia wasio na hatia. 

Mashambulizi yaliyotelekezwa katikati mwa Mogadishu yamesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 26. Kundi la kigaidi la al Shabab lenye makao yake nchini Somalia limetangaza kuhusika na mashambulizi hayo. Kundi hilo limewakamata mateka watu 32 baada ya kutekeleza mashambulizi hayo. 

0 comments:

Post a Comment