Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Iran amekutana na mawaziri wa nchi za Kiafrika mjini Geneva na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kutoa huduma za kiufundi na kihandisi katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano kwenye nchi mbalimbali za Afrika.
Waziri Mahmoud Vaezi ameyasema hayo katika mazungumzo yake na mawaziri wa baadhi ya nchi za Afrika katika kikao kilichofanyika leo kandokando ya Mkutano wa Kimataifa wa Jamii ya Mawasiliano nchini Uswisi.
Amesisitiza juu ya nafasi muhimu ya mawasiliano na teknolojia mawasiliano katika ustawi wa nchi mbalimbali na mchango wake katika kutayarisha nafasi za ajira na kuimarisha uchumi na kuongeza kuwa, kwa sasa makampuni ya kuzalisha zana na vifaa vya mawasiliano ya Iran yanapeleka bidhaa zao katika baadhi ya nchi za Afrika na kwamba, kuna uwezekano wa kupelekwa programu (software) za Iran katika nchi za Kiafrika.
Vaezi pia ameeleza utayarifu wa Jamhuri ya Kiislamu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya pamoja na kutoa mafunzo kwa nguvu kazi hodari na watalamu katika nchi za Afika.
0 comments:
Post a Comment