Home »
Kimataifa
» Kim Jong-un akutana na ujumbe kutoka Korea Kusini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anaandaa mkutano wa chakula cha jioni na wajumbe wawili kutoka Korea Kusini, ikiwa ndiyo mara ya kwanza kiongozi huyo anakutana na ujumbe kutoka Kusini tangu aingie madarakani mwaka 2011.
Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap, liliripoti kuhusu mkutano huo likimnukuu msemaji wa rais nchini Korea Kusini.
Ujumbe huo uko nchini Korea Kaskazini kwa mazungumzo yasiyo ya kawaida yenye lenngo la kuanzisha mchakato kati ya Korea Kaskazini na Marekani.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeboreka kufuata mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi.
Ujumbe huo unawajumuisha maafisa wenye vyeo vya mawaziri - mkuu wa ujasusi Suh Hoon na mshauri wa usalama wa taifa Chung Eui-yong.
Awali Bw Chung aliwaambia waandishi wa habari kuwa atawasilisha azimio la Rais Moon Jae-in la kudumisha mazungumzo na kuboresha uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Kusini na kuondoa silaha za nyuklia kutoka Rasi wa Korea.
Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumapili kuwa Marekani itakuwa tayari kukutana na Korea Kaskazini lakini akasisitiza kuwa Korea ni lazima iondoe zana zake za nyuklia.
Hata hivyo Korea Kaskazini ambayo imesema inataka kufanya mazungumzo na Marekani, imesema kuwa ni hatua ya "kishenzi" kuwa Marekani inataka kuwepo masharti.
Haijulikani ni nani atawakilisha Marekani ikiwa mkutano kama huo utafanyika.
Mjumbe mkuu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini Joseph Yun alitangaza uamuzi wake wa kustaafu mapema wiki iliyopita.
Wadadisi wanaamini kuwa Bw Yun alikuwa akipendelea sana suluhu ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.
Related Posts:
Waliomuingiza mtu mweusi kwenye jeneza, Mahakamani Afrika KusiniHatimaye wakulima wawili weupe wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini, kwa tuhuma za kumsukuma mtu mmoja mweusi na kumuingiza ndani ya jeneza, huku wakitishia kummwagia mafuta ya petroli ili kumteketeza kwa m… Read More
Historia ya Che GuevaraKama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini… Read More
JOSEPH KABILA Tutaendelea kuzungumzia hali ya kisiasa kufikia muafaka Afrika Kusini imeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC pamoja na wanasiasa wa upinzani kuendeleza mazungumzo yenye lengo la kupata muafaka wa kisiasa katika taifa hilo.Rais Jacob Zuma ametoa rai h… Read More
China yaanza kuzipatanisha Afghanistan, PakistanRais Ashraf Ghani na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi.… Read More
Nyuki ‘wamlazimisha’ mshukiwa kujisalimisha KenyaTaarifa kutoka magharibi mwa Kenya zinasema kuwa mtuhumiwa wa wizi wa gari alijisalimisha kwa polisi baada ya kuvamiwa na nyuki akiliendesha gari hilo.Mwandishi wa BBC, Wanyama wa Chebusiri kutoka Nairobi, anasema ripoti hiyo… Read More
0 comments:
Post a Comment