Wednesday 28 February 2018

Ukaguzi wa magari binafsi kuanza rasmi kesho


Leo februari 28, 2018 Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha, Kamanda Charles Bukombe amesema siku ya kesho Machi 1, 2018 wataanza ukaguzi rasmi wa magari ya watu binafsi(private cars) ambao kwa muda mrefu waliusitisha toka mwaka jana mwezi wa kumi, gharama ya ukaguzi huo itakua ni 3000tu.

Kamanda Bukombe na wafanyakazi wa Radio5

Kamanda huyo wa usalama barabarani ameyasema hayo baada ya kutembelea kituo cha Radio5fm katika kipindi cha Funiko Base kinachorushwa kila siku jumatatu-Ijumaa

Kamanda Bukombe amesema katika ukaguzi wao wakibaini gari lako ni bovu wataondoa Plate number na kukuruhusu ukatengeneze gari lako na baada ya hapo utarudisha gari lako tena lihakikiwe kama watajiridhisha watakurudishia Plate number yako.

0 comments:

Post a Comment