Sunday 18 February 2018

Shyrose Bhanji kuhusu mwanafunzi aliyepigwa risasi ‘Serikali ya CCM haiwezi kukwepa lawama



Kukiwa bado na taharuki miongoni mwa Watanzania kuhusu Mwanafunzi wa chuo cha NIT aliyepigwa risasi kwenye maandamano, Hatimaye aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji ametoa ya moyoni na kuweka wazi msimamo wake juu ya tukio hilo na kusema kuwa chama chake cha CCM na serikali haviwezi kukwepa lawama.

Bhanji amesema  kuwa tukio hilo linamfanya ashindwe kula wala kulala kwani ameuawa kikatili na hakua na hatia yoyote ile.

“Serikali ya chama changu CCM haiwezi kukwepa lawama kwa namna yoyote ile kufuatia kupigwa risasi kwa binti ambaye hakuwa na hatia hata kidogo. Imekuwa ni siku mbaya sana kwangu; nimeshindwa kula na nashindwa kupata usingizi kutokana na kifo cha huyu binti. Nafsi yangu inanisuta. Mungu wangu naomba unisaidie,“ameandika Bhanji kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina la Aqulina Akwilini alipigwa risasi na jeshi la polisi Februari 16, 2018 katika eneo la Mkwajuni -Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati jeshi la polisi likiwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment