Alianza Wayne Rooney kufungua ukurasa wa mabao huku likiwa bao lake la 12 dhidi ya Arsenal katika Epl na la 15 katika michuano yote, idadi inayomfanya kuwa mchezaji ambaye amewafunga zaidi Arsenal katika Epl.
Lakini Nacho Monreal aliwasawazishia Arsenal kabla ya Mesut Ozil kuwafungia bao la pili kwa kichwa na kuwafanya Arsenal kuwa timu yenye mabao mengi kwa kichwa tangu msimu uliopita kuanza, wana mabao 23.
Alexis Sanchez aliwafungia Arsenal bao la tatu bao ambalo linamfanya kuwa mchezaji kutokea Ufaransa mwenye mabao mengi zaidi mwaka 2017 ambapo hadi sasa anakuwa amefunga mabao 27.
Aaron Ramsey alifunga bao la nne na Alexis Sanchez akafunga bao la tano na kuwafanya Arsenal kuwa timu ya kwanza kufunga mabao mengi zaidi dhidi ya timu moja baada ya leo kufikisha idadi ya mabao 100 dhidi ya Everton
0 comments:
Post a Comment