Mauritania ni nchi inayo patikana upande wa kaskazini magharibi mwa bara letu tukufu la Afrika.Katika nchi hii wanaume huwanenepesha wake pamoja na binti zao.
Zoezi hili la kuwanenepesha wake pamoja na mabinti hufanywa kwa kutumia dawa za mitishamba, vyakula na vinywaji mbalimbali.
Kwa upade wa mabinti, zoezi hili hufanyika binti anapokuwa ametimiza miaka saba hadi kumi na mara nyingi hufanyika wakati wa likizo.
Mabinti hawa huwekwa katika camp maalumu ambako hutakiwa kula vyakula, vinywaji na mitishamba ya aina mbalimbali iliwaweze kunenepa.
VYAKULA WANAVYO LISHWA
Mabinti hawa hulishwa vyakula vya aina mbalimbali. Baadhi ya vyakula hivyo ni kama ifuatavyo :
1. Vyakula vyote vitamu vitamu na vyenye sukari nyingi
2. Vyakula vyenye mafuta mengi
3. Uji wa ulezi
4. Uji wa ufuta
5. Asali ya tende ( Date Syrup )
6. Maziwa ya mbuzi
7. Maziwa ya ngamia
8. Mitishamba ya aina mbalimbali ambayo husaidia kunenepesha mwili
9. Vyakula vyenye ngano kwa wingi, pamoja na vyakula vya wanga kwa wingi.
9. Pamoja na vyakula vingine vya aina tofauti tofauti ambavyo vinahusika na kumfanya mtu anenepe.
Zoezi hili hufanyika kwa umakini mkubwa bila kuleta utani wa aina yoyote ile. Matrons wanao simamia zoezi hili, huwa wanakuwa serious sana ili kuhakikisha kila mtoto wa kike alie kwenye camp anakula na kutumia kiasi cha chakula na mitishamba anayo takiwa kuitumia kwa kipindi kilicho elekezwa.
Na ikitokea binti akaleta ubishi, basi atalishwa kwa lazima na ikitokea binti huyo akajitapisha chakula, kinywaji au kimiminika cha mitishamba alicho pewa kutumia, basi matrons watamtisha kwamba, endapo atatapika, atalazimishwa kula matapishi yake.
Zoezi hili huendelea pindi binti anaporudi nyumbani kwa wazazi wake na hufanyika kila siku hadi utakapo fika wakati wake wa kuolewa.
Akiwa kwa wazazi wake, binti atatakiwa kuwa anatumia kila siku vimiminika vinavyo tokana na mitishamba inayo saidia kunenepesha mwili pamoja na vinywaji & vyakula, vinavyo saidia kunenepesha mwili.
Zoezi hili hufanyika kwa umakini mkubwa sana. Wazazi wa wabinti huwa makini na wakali katika kuhakikisha binti yao anazingatia kutumia vyakula hivyo pamoja na mitishamba hiyo ya kunenepesha mwili.
BAADA YA KUOLEWA
Hata baada ya kuolewa, mwanamke huyo hutakiwa kuendelea kutumia vyakula na mitishamba ya kunenepesha on daily basis. Mume huwa makini sana na humsisitizia mkewe kutumia mitishamba na vyakula vya kunenepesha.
NI UTAMADUNI WAO TOKA KALE
Kuwalazimisha mabinti pamoja na wake kutumia vyakula na mitishamba ya kunenepesha mwili, ni utamaduni wa watu wa Mauritania tangu enzi na enzi.
Zoezi hili hufanyika kama sehemu ya kuenzi utamaduni huo ulio jikita mizizi miongoni mwa wananchi wa Mauritania.
SABABU GANI HUWAFANYA WANAUME WA MAURITANIA KUWANENEPESHA BINTI ZAO NA WAKE ZAO.
Sababu kuu inayo wafanya wanaume wa Mauritania kuwanenepesha wake na binti zao ni dhana iliyo jengeka
i. Dhana iliyo jengeka miongoni mwa jamii ya wana Mauriutania kwamba, mwanamke mnene ndio mrembo. Kwa wana Mauritania, ili mwanamke aweze kuonekana mrembo ni lazima awe mnene.
Kama sio mnene basi hawezi kuchukuliwa kama mrembo na ni vigumu sana kuolewa.
Pindi kijana anapo peleka taarifa kwa wazazi wake kwamba amepata mchumba na kwamba anataka kumuoa, swali la kwanza analo ulizwa ni kama mwanamke huyo ni mnene au la, na kama mwanamke huyo si mnene, basi familia nzima wataipinga na kuisusia ndoa hiyo.
Hivyo basi katika kuhakikisha mabinti zao wana fit in kwenye jamii, wana Mauritania huhakikisha kuwa binti zao wanakuwa wanene kwa kufanya zoezi hilo la kuwanenepesha tangu wakiwa wadogo.
ii. Sababu ya pili ni FAHARI kwa wazazi na mume. Baba na mama mzazi ni fahari kwao kumuoza binti yao akiwa mnene vilevile mume ni fahari kwake kuwa na mwanamke mnene na pia kuendelea kudumisha unene wake hata baada ya kufunga ndoa.
Kwa wana Mauritania wengi, unene ni ishara ya kuwa na maisha mazuri yenye neema. Ishara ya kutokuwa na njaa. Hivyo basi kuruhusu binti au mke wako kukonda, itakufanya uonekane wewe hauna maisha mazuri.
Hauna uwezo wa kuwatunza binti zako na mke wako.
Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na haki za wanawake yamekuwa yakijitokeza hadharani kupingana na desturi hii, lakini bila mafanikio kwani imethibitika kuwa wana Mauritania wengi bado wana amini katika desturi hii na kwamba ni vigumu sana kuiacha kwa mara moaja.
KUNENEPA NI RAHISI SANA KULIKO KUPUNGUA
Kunenepa ni rahisi kuliko kupungua. Duniani hakunaga mtu mwembamba. Uzoefu unaonyesha kuwa, mtu anae taka kunenepa anaweza kupata matokeo ya haraka zaidi kuliko Yule anae taka kupungua.
Hii ni kwa sababu njia za kunenepa ni rafiki zaidi kwa mtu anaetaka kunenepa kuliko ilivyo kwa njia za kupungua mwili.
Kwa mfano, mtu anaetaka kupungua pamoja na mambo mengi kama kutumia dawa, anaweza kutakiwa pia kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kufanya diet na kuachana na baadhi ya vyakula, jambo ambalo ni tofauti na mtu anaetaka kuongeza na kunenepesha mwili.
LISHE YA KUNENEPESHA MWILI
Kama mwili wako ni mwembamba au umedhoofika kutokana na maradhi ya sababu mbalimbali kama vile stress nakadhalika, ipo DAWA LISHE YA KUNENEPESHA MWILI. Dawa hii ni ya asili na itasaidia kunenepesha mwili wako na kuurudisha katika hali yake ya kawaida.
0 comments:
Post a Comment