Jana nimepokea barua kuwa shamba la mvomero ekari 326 limetwaliwa na rais na sitakiwa kukanyaga hapo. Shamba hilo lina majengo, mazao, mashine mbali mbali, visima virefu vya maji, umeme na mifugo mchanganyiko zaidi ya 200. Kisingizio shamba halijaendelezwa! Shamba lenye vitu vyote hivyo halijaendelezwa??
Mbaya zaidi katika kupinga dhamira hizo nilifungua kesi mahakama kuu kwa mashamba yote na mahakama zimeweka zuio la kutokuingiliwa mashamba hayo mpk mashauri ya msingi yatakapoamuliwa.
Lakini wameshaamua kwa hiyo mahakama hazina kazi. Utawala huu haufuati sheria ni udikteta mtupu! Kuna mwana ccm moja alisema "tutamfilisi mpk atakapotembelea ndala ndo atakumbuka kurudi ccm."
Hilo litawezekana kama Mungu huyu ni wa ccm. Ccm sirudi pamoja kuwa najua nitateseka na familia yangu! Kisasi hiki mimi sitakiweza namwachia Mungu ndiye atakayetufuta machozi mimi na familia yangu."
FREDRICK TLUWAY SUMAYE.
WAZIRI MKUU MSTAAFU.
Source: JF
0 comments:
Post a Comment