Home »
KITAIFA
» ZITTO Kabwe Awaamshia DUDE Chadema.......
KIONGOZI Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, katika kile kilichoonekana kuwapa kijembe Chadema, akisema kutaka nchi kunyimwa misaada ni uhayawani, kwani vita dhidi ya kuminywa kwa demokrasia inapaswa kupiganwa ndani.
Zitto alitoa kauli hiyo kupitia akaunti yake katika Mtandao wa Kijamii wa Twitter, ikiwa ni siku moja tu baada ya Chadema kupitia kwa mwanasheria wake, Tundu Lissu kuitaka Jumuia ya Kimataifa kuinyima Tanzania misaada kufuatia kitendo cha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa viongozi wa upinzani, hasa kutoka chama chao.
“Huu ni uhayawani, hii ni nchi huru, kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa, tupambane ndani kuleta demokrasia,” aliandika Zitto.
Hata hivyo, kufuatia kauli hiyo baadhi ya watumiaji wa mtandao huo walianza kumuuliza maswali kadha Zitto ambaye aliwajibu na kuufanya mjadala huo kuwa mrefu, baadhi wakimuunga mkono na wengine wakipingana naye.
Related Posts:
Makosa dhidi ya binadamu yaongezeka kwa asilimia 0.9Jeshi la Polisi limesema makosa dhidi ya binadamu yanayojumuisha mauaji, kubaka, kulawiti, kunajisi, wizi na kutupa watoto na usafirishaji binadamu yameongezeka nchini.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert … Read More
Serikali yatangaza ajira mpya za walimu.
Serikali imetangaza kutoa ajira mpya za walimu wa shule za msingi na sekondari hii leo, ambapo jumla ya walimu 3033 wamechaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa… Read More
Sugu awashangaa wanachama wa CCMMbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amewashangaa wananchama wa CCM waliolipigia hesabu jimbo hilo, akidai kuwa wanajisumbua kwa sababu walishapoteana tangu mwaka 2010.Akizungumza leo Desemba 20 katik… Read More
Wanaohubri kwenye mabasi kukiona cha motoBaraza la Ushauri wa watumiaji wa huduma za safiri wa nchi kavu na majini, SumatraCCC limekitaka chama cha wamiliki wa mabasi nchini TABOA na washirika wao kuhakikisha wanasimamia vyema suala la baadhi ya watu kugeuza magari … Read More
Tambwe Hizza Kuzikwa Leo Makaburi ya Chang'ombeMWILI wa Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Richard Tamilway maarufu kwa jina la ‘Tambwe’ aliyefariki dunia jana asubuhi nyumbani kwake Mbagala Kizuiani, unatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi katika Makabur… Read More
0 comments:
Post a Comment