Picha ya Pamoja na Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Waandishi wa habari,Watangazaji toka Kanda ya Kaskazini na Mameneja wa mamlaka ya hali ya hewa toka katika Kanda mbalimbali Tanzania,wamekutana kwa siku tatu na kupatiwa elimu Juu ya utoaji na uwasilishaji wa taarifa ya hali ya hewa.
Semina hiyo ya siku tatu iliyo simamiwa na wawezeshaji toka Farm Radio International imewawezesha Mameneja wa Kanda wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania kujifunza zaidi utoaji wa taarifa za hali ya hewa kwenye vyombo vya habari.
Akifunga Semina hiyo ya siku tatu Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania amesema ana matumaini makubwa kuwa elimu waliyo ipata itawawezesha Mameneja kuweza kutoa taarifa za hali ya hewa ipasavyo.
Dr Kijazi amesema mamlaka ya hali ya hewa kutoa taarifa bila kumfikia mlengwa kwa wakati muafaka inakuwa haina maana.
Dr Kijazi amesema ni muhimu kwa walengwa kujua taarifa za hali ya hewa hususani Wakulima ili waweze kubadilika kulingana na taarifa za utabiri wa hali ya hewa.
Amewataka waandishi kuwa huru kutembelea ofisi za mamlaka ya hali ya hewa katika Kanda na katika ofisi za makao makuu ili kupata taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa undani zaidi.
Mafunzo hayo yaliwapa uwezo watangazaji na Wataalamu kufanya mazoezi mbalimbali ya utabiri wa hali ya hewa kwa vitendo zaidi.
Mazoezi ya vitendo yakifanyika,Mtangazaji,Mtaalamu wa Mamlaka ya hali ya hewa,Mtaalamu wa Masuala ya Kilimo na Mkulima
Picha ya pamoja ya waandishi na watangazaji toka katika vituo mbalimbali Kanda ya Kaskazini.
Kwa taarifa zaidi sikiliza kipindi cha Good morning Tanzania cha Radio 5,Jumatatu kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne kamili asubuhi.
PICHA NA TAARIFA ZAIDI ENDELEA KUFUATILIA BLOGU HII.
0 comments:
Post a Comment