Home »
KITAIFA
» Tundu Lissu Akamatwa Akiwa Uwanja wa Ndege Akijiandaa Kwenda Rwanda
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa leo, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.
Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martn Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi.
Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kwamba mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii.
Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kwamba ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Related Posts:
Tundu Lissu Apandishwa Mahakamani na Kusomewa Mashtaka Haya...Uwezi Amini Mawakili 21 Wamejitokeza KumteteaMbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (KATIKATI), alivyofikishwa mahakamani leo.Baada ya kuwekwa mahabusu kwa siku nne, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu leo amefikishwa Ma… Read More
Alichokiongea Kikwete leo Julai 24, 2017Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema kuwa ipo haja ya kuzalisha wataalamu zaidi ili kukwepa kupeleka wagonjwa nje ya nchi.Amesema hayo leo Jumatatu, Julai 24, alipokuwa akizindua mkutano wa siku mbili uliozikutanisha … Read More
Werema afunguka kwanini alimuita Kafulila ‘Tumbili’Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema amezungumzia kauli yake ya mwaka 2014 ya kumuita ‘tumbili’ aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila wakati wa mjadala wa Escrow bungeni, ambapo amesema uli… Read More
Ukweli Mchungu: Siku Hizi Wazee Wako Shapu Kuliko Vijana, Rais Magufuli AfungukaRais Magufuli amesema siku hizi siyo vijana peke yao wanao haribu wanafunzi, na kwamba wapo wazee walioko shapu na hawapitwi kuwapa mimba wanafunzi, na kuwataka wenye tabia hiyo waache kwa sababu watafungwa kwa miaka 30.Rais … Read More
ADC Wajitosa kwa Rais Magufuli, Waomba Abadili Msimamo wakeChama cha ADC kimemwomba Rais Magufuli katika miaka hii mitatu iliyobaki kubadilisha msimamo wa kuzuia kufanywa kwa mikutano ya hadhara inayotakiwa kufanywa na vyama vya upinzani.Akizungumza katika kuelekea maadh… Read More
0 comments:
Post a Comment